Shirikisho la Mpira wa Kikapu Duniani (FIBA)
limetangaza kuafiki pendekezo la Iran la kutaka wanawake wa Kiislamu na
mabinti wenye Hijabu wa Kiirani kushiriki katika michezo ya kimataifa ya
mpira wa kikapu (basketiboli).
Mahmoud Mashhoon Mkuu
wa Shirikisho la Mpira wa Kikapu la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran
ametangaza kuwa, hatimaye Shirikisho la Mpira wa Kikapu Duniani (FIBA)
limekubaliana na matakwa ya Iran ya wachezaji wake wa kike kushiriki
katika mashindano ya kimataifa ya mpira wa kikapu wakiwa wamejistiri kwa
vazi tukufu la Hijabu.
Ameongeza kuwa, uamuzi huo wa FIBA
umetangazwa katika kikao cha shirikisho hilo kilichofanyika huko Hong
Kong. Mkuu wa Shirikisho la Mpira wa Kikapu la Jamhuri ya Kiislamu ya
Iran amesema kuwa, kufuatia uamuzi huo, kuanzia Oktoba mwaka huu mabinti
wa Kiirani sasa wataweza kushiriki katika mashindano ya kimataifa ya
mchezo huo wakiwa wamejistiri kwa vazi la Hijabu.
Ikumbukwe kuwa, Timu ya Taifa ya
Wanawake ya Mpira wa Kikapu ya Jamhuri ya kiislamu ya Iran kwa muda sasa
haikuwa ikishiriiki katika mashindano ya kimataifa ya mpira wa kikapu
kutokana na Shirikisho la Mpira wa Kikapu Duniani (FIBA) kupiga marufuku
wanawake wanaovaa Hijabu kushiriki katika mashindano yanayoandaliwa na
shirikisho hilo.
Shirikisho la Mpira wa Kikapu Duniani
(FIBA) lililazimika kuanzisha mchakato wa kuangalia uwezekano wa
kuruhusiwa vazi la Hijabu baada ya shirikisho hilo kupokea malalamiko
kutoka nchi kadhaa kufuatia marufuku yake ya Hijabu katika mashindano ya
kimataifa yanayoandaliwa na shirikisho hilo.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.