ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Monday, August 21, 2023

TAMKO LA KAMATI YA AMANI MKOA WA MWANZA KUHUSU BANDARI

 NA ALBERT G. SENGO/MWANZA

KAMATI ya Amani ya Viongozi wa Dini Mkoa wa Mwanza, inayoundwa na viongozi mbalimbali hii leo asubuhi imetoa tamko lake ikiishauri jamii kutumia busara katika kuyazungumzia masuala ya mkataba wa bandari, sanjari na kuiomba Serikali kuandaa makongamano ya elimu kwa wananchi ili kutoa maoni yao kwenye marekebisho ya vipengele vinavyoleta utata ndani ya mkataba huo tofauti na sasa ambapo kila mmoja anazungumza kivyake kwa lugha ngumu na zenye hasira mitandao bila muongozo.
Tamko hilo hilo lilitolewa mbele ya waandishi wa habari na Wenyeviti Wenza wa Kamati hiyo Askofu Dk. Charles Sekelwa na Sheikh Hasani Kabeke.


Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.