Waziri wa zamani w Rwanda, Jacques Bihozagara ameaga dunia akiwa katika jela ya Burundi yapata miezi minne baada ya kutiwa nguvuni kwa tuhuma za kufanya ujasusi.
Jacques Bihozagara ambaye aliwahi kuwa waziri wa vijana wa Rwanda na balozi wa nchi yake katika nchi za Ubelgiji na Ufaransa alitiwa nguvuni December 4, 2015 na Shirika la Upelelezi la Taifa la Burundi (National Intelligence Service (SNR)) linalodhibitiwa moja kwa moja na Rais Pierre Nkurunziza wa Burundi. Bihozagara ambaye amefariki dunia katika jela ya Mpimba mjini Bujumbura, alikuwa akikabiliwa na tuhuma za kufanya ujasusi kwa maslahi ya shirika la ujasusi la Rwanda.
Wizara ya Mambo ya Nje ya Rwanda imetangaza kuwa imeshtushwa na habari ya kifo cha mwanadiplomasia huyo wa zamani na kusisitiza kuwa, serikali ya Burundi inapaswa kutoa majibu kuhusu mazingira na sababu za kifo chake.
Uhusiano wa Rwanda na Burundi ulivurugika baada ya Rais Nkurunziza kuituhumu Rwanda kwamba inawasaidia waasi wanaotaka kuiondoa madarakani serikali yake. Rwanda inakanusha madai hayo.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.