Tazama MO tv, kuona tukio hilo hapa:
Taasisi isiyo ya kiserikali T-MARC Tanzania imezindua rasmi jengo lake jipya pamoja na ghala maalum la kisasa litakalotumika kuhifadhia bidhaa zao ikiwemo zile za mipira ya kiume na kike kupitia bidhaa zao za DUME.
Tukio hilo limefanyika rasmi mapema jana Aprili 1.2016, ambapo Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamisi Andrea Kigwangalla alikuwa mgeni rasmi akiwakilisha Serikali katika tukio hilo kubwa na la kihistoria.
Akizungumza na wanahabari, Naibu Waziri wa Afya Dk. Kigwangalla amebainisha kuwa, Serikali inapongeza juhudi za Taasisi za watu binafi ikiwemo T-MARC Tanzania wanavyofanya juhudi kubwa hapa nchini katika kuwafikia wananchi kupitia bidhaa zao hizo za kinga.
Dk. Kigwangalla amewapongeza kwa hatua hiyo tokea walipoanza hapa nchini kuanzia mradi hadi taasisi ambapo kwa hatua yao hiyo pia imesaidia na mapambano ya virusi vya UKIMWI kwani kupitia bidhaa zao hizo za kondomu kupitia kondomu za DUME zimekuwa msaada mkubwa sana kazi hizo wanazofanya wanaisaidia Serikali kwa kiwango kikubwa sana.
Kwa upande wake, Mkurugenzi mtendaji wa T-Marc Tanzania, Bi.Diana Kisaka alishukuru Serikali ya Tanzania kwa kushirikiana na taassi hiyo kwani imeweza kutimiza malengo yake hapa nchini na itaendelea kushirikiana na Serikali bega kwa bega kwa kipindi chote.
Aidha, aliongeza kuwa, wataendelea kutoa huduma bora hiyo ya kinga kupitia bidhaa zao za mipira ya kinga yaani kondomu za DUME ilikuzuia mapambano ya virusi vya UKIMWI hapa nchini.
Awali Dk. Kigwangalla alipata wasaha wa kukagua mabanda ya maonyesho ya miradi mbalimbali ya taasisi hiyo na kupata maelezo ya kwa kina kisha alipata wasaha wa kufungua rasmi jengo hilo la kisasa ambalo ni la ofisi za taasisi hiyo pamoja na kuzindua ghala maalum la kuhifadhia bidhaa hizo za DUME Condom.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamisi Andrea Kigwangalla akisalimiana na Mjumbe wa bodi ya T-MARC Tanzania, Bi Joyce Mhavile wakati wa kuwasili katika eneo la tukio hilo la ufunguzi rasmi wa jengo la kisasa la makao makuu ya T-MARC Tanzania yaliyopo Jijini Dar es Salaam.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamisi Andrea Kigwangalla akimsikiliza Meneja Mradi wa T-MARC Tanzania, Bi. Halima Mwinyi wakati wa kutembelea miradi ya kwenye mabanda ya maonyesho kwenye tukio hilo la ufunguzi rasmi wa jengo la kisasa la makao makuu ya T-MARC Tanzania yaliyopo Jijini Dar es Salaam.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamisi Andrea Kigwangalla akimsikiliza afisa wa T-MARC Tanzania, Bi. Sophia Komba wakati wa kutembelea miradi ya kwenye mabanda ya maonyesho kwenye tukio hilo la ufunguzi rasmi wa jengo la kisasa la makao makuu ya T-MARC Tanzania yaliyopo Jijini Dar es Salaam.
Jengo jipya la T-MARC Tanzania kabla ya uzinduzi huo linavyoonekana
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamisi Andrea Kigwangalla akikata utepe kuashiria kulifungua rasmi jengo hilo la kisasa la makao makuu ya T-MARC Tanzania yaliyopo Jijini Dar es Salaam.
Jiwe la msingi la ufunguzi wa jengo hilo
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamisi Andrea
..Dk. Kigwangalla akitembezwa katika maeneo mbalimbali ya jengo hilo..
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamisi Andrea
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamisi Andrea Kigwangalla akifungua kitambaa kuashiria ufunguzi wa jengo la kuhifadhia bidhaa ya taasisi hiyo ghala maalum
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamisi Andrea Kigwangalla akiangalia ghala hilo kwa ndani namna lilivyojengwa .
Dk.Kigwangalla akiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa taasisi hiyo ya T-MARC Tanzania.
Dk.Kigwangalla akiwa katika picha ya pamoja na wadau na wadhamini wa taasisi hiyo ya T-MARC Tanzania.
Dk.Kigwangalla akiwasili katika eneo maalum la kutolea hotuba ya tukio hilo.
Mkurugenzi mtendaji wa T-Marc Tanzania, Bi.Diana Kisaka akitoa hotuba fupi ya ufunguzi huo
Mwanamuziki Barnaba akitoa burudani katika tukio hilo..
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamisi Andrea Kigwangalla akitoa hutuba katika tukio hilo
mjumbe wa bodi, Bw.Alex Mgongolwa akitoa shukrani zake
Uongozi wa T-MARC Tanzania wakitoa zawadi maalum ya picha ambayo yenye kuonyesha mwanamke akiwa na mtoto katika malezi bora iliyoelezewa kwa njia ya sanaa
Wadau wakifuatilia tukio hilo
Dk. Kigwangalla akipata picha ya pamoja na wadau katika tukio hilo
Baadhi ya wafanyakazi wa taasisi ya T-MARC Tanzania wakifurahia katika tukio hilo
Bi. Teddy Mapunda akijadiliana jambo na Katibu wa Naibu Waziri wa Afya Bw. Kulwa.Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamisi Andrea Kigwangalla akiagana na Mkurugenzi mtendaji wa T-Marc Tanzania, Bi.Diana Kisaka wakati akiondoka katika eneo la tukio hilo la ufunguzi rasmi wa jengo la kisasa la makao makuu ya T-MARC Tanzania yaliyopo Jijini Dar es Salaam. (Picha zote na Andrew Chale,Modewjiblog).
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.