Wanafunzi wa shule ya msingi ya Zawa wilaya ya Maswa mkoani Simiyu wanalazamika kusoma madarasa matatu katika chumba kimoja kwa kupeana migongo na kutumia mbao mbili tofauti wakati walimu wakifundisha kutokana na changamoto ya vyumba vya madarasa ambapo shule hiyo ina vyumba vitatu yenye wanafunzi 513.
Mbunge wa Jimbo la Maswa Magharibi Mashimba Ndaki ameshuhudia vyumba hivyo na idadi ya wanafunzi kwa mujibu wa Mwalimu Mkuu Wiliam Timothy kufuatia ziara yake na kujionea changamoto kupitia wajumbe wa Serikali za vijiji na mikutano ya hadhara ikiwa ni mara yake ya pili kufika shuleni hapo na kuweza kuahidi saruji ya ujenzi wa nyumba ya mwalimu.
Aidha Mbunge huyo amewapongeza wananchi kwa nguvu kazi ya ujenzi wa vyumba vitatu vya madarasa vilivyofikia hatua ya Renta ,ufiatuaji wa matofali na mchanga wa ujenzi wa nyumba ya mwalimu hali ambayo itapunguza tatizo la watoto kusoma wakiwa wamebanana na walimu watano kuishi katika nyumba moja na kuahidi mabati 160 kwaajili ya kuezeka jengo hilo na saruji mifuko 50,huku akisisitza dhana ya ushirikishwaji wananchi katika shughuli za maendeleo.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.