- Airtel yazindua duka Mbagala, Yatangaza kuzindua maduka mengine 10 kwa mwezi
- Airtel kufungua maduka mapya Babati, Sumbawanga, Tegeta, Mpanda, Kigoma, Shinyanga, Singida, Musoma, Songea, na LindiKampuni ya simu za mkononi ya Airtel imezindua duka jipya la kisasa jijini Dar es salaam Mbagala ikiwa ni muendelezo wa kukamilisha mkakati wake wa kutoa huduma na bidhaa bora za mawasiliano kila mahali nchini.Uzinduzi wa duka jipya la Airtel Mbagala uko katika mkakati waliojiwekea Airtel ambapo hadi sasa wamefanikiwa kujenga maduka mapya 6 katika mikoa ya Tanga, Moshi, Kariakoo, Kahama, Mwanza ndani ya Rock City Mall pamoja na duka la Airtel Expo lililopo makao makuu ya Airtel Moroko jijini DSM. Sambamba na hilo Airtel imekarabati maduka yake yote nchini ili kutoa huduma zinazoendana na karne ya sasa katika sekta ya mawasilianoAkizindua hilo Mbagala jijini Dar es salaam Mkuu wa wilaya ya Temeke Bi Sophia Mjema aliipongeza Airtel na kuwataka wakazi wa Mbagala na maeneo ya jirani kulitumia vyema duka hilo katika kupata huduma za mawasiliano kwa kuwa mawasiliano sasa yanachangia sana katika maendeleo ya jamii“Ninawapongeza sana Airtel kwa ha kufungua duka hapa MBAGALA, ninatambua huduma ya mawasiliano ni chachu ya maendeleo ya jamii na nchi kwa ujumla, tunajionea jinsi baadhi ya huduma za kimtandao kama Airtel Money zilivyo na usalama kwa jinsi zinavyowawezesha watumiaji hata kutunza pesa zao, kulipia ankara mbalimbali, kutuma na kupokea pesa pamoja na kujipatia mikopo kama ilivyo huduma ya kipekee ya mikopo isiyo na masharti ijulikanayo kama Airtel TIMIZA sasa”.
- “Nitoe wito sasa kwa wakazi wa MBAGALA, sasa tumieni duka lenu hili la karibu kujipatia huduma mbalimbali, kusajili namba za simu pamoja na kuzihakiki ili kutimiza maagizo ya serikali ya kwamba kila anaetumia namba ya simu iwe imesajliliwa kwa jina lake ili kupunguza uhalifu”.
Nae Mkurugenzi wa huduma kwa wateja wa Airtel Bi Adriana Lyamba alisema “ huduma zitakazotolewa ni pamoja na kukusanya Ankara, kurudisha namba zilizopotea, mauzo ya simu za kisasa na ORIGINAL, Airtel money-kutoa na kuweka fedha, kuunganisha wateja na Intaneti ya Airtel pamoja na huduma zote za kimtandao .
“katika muendelezo wa dhamira yetu ya kutoa huduma karibu zaidi na wateja wetu baada ya uzinduzi wa Duka hili hapa Mbagala Airtel tumeijipanga kufungua maduka mengine zaidi ya 10 yajulikanayo kama Airtel Xpress Shop katika katika maeneo ya Tegeta, Babati, Sumbawanga, Mpanda, Kigoma, Shinyanga, Singida, Musoma, Songea, na Lindi” alieleza Bi, Lyamba
Duka la Airtel Mbagala litakuwa likitoa huduma kuanzia saa 3 asubuhi hadi saa 11 na dakika 30 jioni kwa siku za Jumatatu hadi Ijumaa na pia siku ya Jumamosi kuanzia saa 4 asubuhi hadi saa 6 za mchana.
1) Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Sophia Mjema (kushoto) na Mkurugenzi wa Huduma kwa Wateja wa Airtel Tanzania, Adriana Lyamba wakikata utepe kuzindua Duka jipya la Airtel, lililopo Mbagala Rangi Tatu, jijini Dar es Salaam jana.
2) Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Sophia Mjema (kushoto) akipata maelezo kutoka kwa Mkurugenzi wa Huduma kwa Wateja wa Airtel Tanzania, Adriana Lyamba (wa pili kushoto), baada ya kuzindua Duka jipya la Airtel, lililopo Mbagala Rangi Tatu, jijini Dar es Salaam jana.
3) Mkurugenzi wa Huduma kwa Wateja wa Airtel Tanzania, Adriana Lyamba (kulia), akitoa maelezo kwa Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Sophia Mjema (kushoto), baada ya mkuu huyo kuzindua Duka jipya la Airtel, lililopo Mbagala Rangi Tatu, jijini Dar es Salaam jana. Katikati ni Meneja wa Duka hilo, Lulu Mashiba.
4) Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Sophia Mjema (wa pili kushoto) akipata maelezo kutoka kwa Mkurugenzi wa Huduma kwa Wateja wa Airtel Tanzania, Adriana Lyamba (kulia), baada ya kuzindua Duka jipya la Airtel, lililopo Mbagala Rangi Tatu, jijini Dar es Salaam jana.
5) Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Sophia Mjema (wa pili kulia) akijadiliana jambo na Mkurugenzi wa Huduma kwa Wateja wa Airtel Tanzania, Adriana Lyamba (kulia), Meneja Uhusiano wa Airtel, Jackson Mmbando (wa tatu kulia), baada ya kuzindua Duka jipya la Airtel, lililopo Mbagala Rangi Tatu, jijini Dar es Salaam jana.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.