NA PETER FABIAN, MWANZA.
HALMASHAURI ya Jiji la
Mwanza kupitia Kamati yake ya Uongozi na Fedha imemsimamisha kazi Mhandisi
wa jiji hilo, Ezekiel Kunyalanyala, kwa tuhuma za kushindwa kusimamia vyema
matumizi ya zaidi ya sh ml 300 fedha za miradi ya maendeleo zilizotolewa kwa
matengenezo ya dharula.
Miradi hiyo ni ya
kukarabatiwa jengo la machinjio ya jiji yaliyopo eneo la Nyakato Kata ya
Mhandu, daraja la Mwananchi lililopo Kata ya Mahina, mitaro ya barabara za Kata
za Mhandu, Mkuyuni na ukarabati wa Kituo cha kulelea watoto waisho katika
mazingira magumu cha zamani kijulikanacho kama Kuleana katika Kata ya Nyamagana.
Akizungumza na waandishi
wa habari leo ofisini kwake Meya wa jiji la Mwanza, James Bwire, alisema kwamba
tayari agizo la Kunyalanyala kusimamishwa kazi limetekelezwa na ameisha
kabidhiwa barua yake kutokana na kushindwa kusimamia matumizi ya fedha za miradi
hiyo ambayo inaonekana kutekelezwa chini ya kiwango kulingana na thamani ya
fedha zilizotolewa.
Meya huyo alieleza kuwa,
Kuleana kilitakiwa kukarabatiwa kwa sh ml 19 kwa ajili ya kutumiwa na Idara ya
Ustawi wa Jamii, lakini badala ya ukarabati ulioelekezwa, kimepakwa rangi na
kuwekwa milango miwili tu na vitasa.
“Mhandisi huyo ndiye
aliyependekeza na kuomba fedha hizo kwa ajili ya ukarabati wa kituo hicho,
haiwezekani sh ml 19 ziishie kupaka rangi, chokaa na kutengeneza milango miwili
tu, badala ya kukarabati sehemu zilizoelekezwa, huo ni wizi tusioweza
kuuvumilia,” alichachamaa Bwire.
Alieleza kuwa, baada ya
Kamati ya Fedha na Uongozi chini ya uenyekiti wake mbali na kutembelea kituo
hicho pia walitembelea miradi ya Machinjio ya jiji yaliyopo Nyakato, Daraja la
Mwananchi na ujenzi wa mitaro ya barabara ya Mhandu, walibaini ujenzi kuwa
chini ya kiwango kulingana na thamani ya fedha zilizotolewa baada ya wataalamu
wa Wizara ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) kuja na
kutembelea kabla ya kuidhinisha kwa matengenezo hayo.
“Halmashauri iliomba
kujengewa machinjio mpya ya kisasa kupitia mradi wa mazingira wa LVMP II kwa
thamani ya sh bl 1.7 kwa sharti la kukarabati jengo moja la stoo ya ngozi
katika machinjio hayo ili litumike kama machinjio ya mda, jiji likakubali na
kutoa sh ml 150 lakini ukarabati huo pia hauendi vizuri,” alidai.
Alieleza miradi mingine
aliyodai na Kamati yake kutoridhishwa na usimamizi wake katika ujenzi wa daraja
la Mwananchi (sh ml 110) na ujenzi wa mitaro ya Mhandu (ml 26) hivyo kumuagiza
Mkurugenzi wa jiji, Adam Mgoyi amwandikie baraua ya kumsimaisha kazi Mhandisi
Kunyalanyala na tayari ameisha kabidhiwa barua ya kusimishwa.
Meya Bwire ambaye pia ni
Diwani wa Kata ya Mahina (CCM) wilayani Nyamagana, alimtaja mtumishi mwingine
aliyesimaishwa kuwa ni Mwanasheria wa jiji hilo, Maksudi Bwabo kutokana na
kulalamikiwa na wadau (wafanyabiashara) wa jiji hilo wakati wa
kukusanya mapato kuwatishia kuwapeleka mahakamani bila kuwapatia nafasi ya
kujitetea.
“Mwanasheria huyo
anadaiwa kutembea na kutoa Samansi mfukoni kutishia wadau hali ambayo tumeomba
akae pembeni “naye kusimamishwa” ili kupisha uchunguzi wa malalamiko ya tuhuma
hizo , pia kuwataka watumishi wa Halmashauri hiyo wabadilike na kuacha kufanya
kazi kwa mazoea ukizingatia kasi ya serikali ya Dk John Magufuli haina mchezo
katika kuwatumikia wananchi.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.