ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Friday, August 3, 2012

TSC SPORTS ACADEMY YATISHA NCHINI UJERUMANI

Nahodha wa TSC Madukuru akimkabidhi zawadi kutoka tanzania, meya wa jiji la Brackenheim nchini Ujerumani.

Badge ya TSC Academy pamoja na Zawadi kinyago kutoka Nyumbani Tanzania aliyokabidhiwa meya

TSC Academy

Salaaam kwa mheshimiwa Meya...

Wachezaji wakipewa zawadi za nguo na meya wa Brackenheim

Miraji Madenge akisaini kwenye kitabu cha wageni

Mkurugenzi wa TSC Mutani Yangwe, Mratibu wa TSC Ujerumani Jurgen Seitz wakifurahia jambo na Meya

Hapa ni kazi tu uwanjani...

TSC yatoa Kipa bora

Licha ya kipindi fulani kuwa katika mapunziko suala la mazoezi kwa timu ya vijana wa Mwanza TSC liko pale pale ndani ya ratiba.

Picha ya msafara mzima wa Timu ya TSC Academy Ulipomtembelea meya wa Brackenheim
Timu ya TSC Sports Academy U20, Yawatoa kamasi Vijana wenzao wa  Ujerumani
Timu ya TSC Sports Academy (U20) ya Jijini Mwanza, Iliyoko kwenye ziara ya michezo hasa mpira wa miguu, Imeendelea kutisha kwa kutoa dozi kwa baadhi ya timu inayokutana nazo kwenye manshindano mbalimbali.

Katika Mashindano ya maarufu ya Insel Cup 2012 yanayofanyika kila mwaka katika mji wa  Mannheim yakishirikisha timu mbalimbali kutoka Ulaya na hapa Ujerumani. Mashindano haya ya timu za miaka 20 yana umri wa miaka 55 toka yaanzishe katika mjii huu. Mashindano ya Mwaka huu yalishirikisha timu za
Maccabi Haifa-U20 ambao ni mabingwa wa vijana inchini Israel, Hijduk Split – U20 Mabingwa wa vijana Croatia, TSC Hoffenheim – U20 ambao wanashiriki na kushka nafasi bora za juu katika msimamo wa ligi ya vijana hapa Ujerumani, 1860 Munich timu ngumu kabisa ya vijana na moja ya timu tano bora hapa Ujerumani, timu nyingine ni wenyeji Waldhof Mannheim-U20 na Karsruher SC zote za hapa Ujerumani.
TSC Academy  Ilipangwa kundi A na timu za Maccabi Haifa, 1860 Munich, TSG Hoffenheim na kundi B lilikuwa na timu za Hijduk Split ya Croatia, Karlsruher na Waldhof Mannheim

Matokeo ya TSC yalikuwa yakuwa kama ifuatavyo:-
Group A
TSC Academy 2 –2 1860 Munich, TSC Academy 1- 1 TSG Hoffenheim, TSC Academy 0- 1 Maccabi Haifa Mshindi group hili alikuwa 1860 Munich  Point 4, akifuatiwa na Maccabi Haifa point 3 na TSC Academy point 2 magoli 3, TSC Hoffenheim Point 2 magoli 2

Na katika msimambo wa Jumly TSC ilishika nafasi ya 5 baada ya kucheza mechi nyingine ambayo tulicheza na Waldof Mannheim na kutoka 1-1.

Kwa ujumla vijana walionyesha mchezo mzuri na kuvutiwa na mawakala na timu zote zilizokuwa katika mashindano, kwa maana ya kwamba TSC Academy ndio timu peek ambayo ilikuwa haishiriki ligi yoyote ya vijana kwetu Tanzania, lakini timu nyingine zinashiriki ligi kuu za vijana za nchi zao, wachezaji wa TSC waliongara sana kwenye mashindano hayo ni Abubakari Hasimu – wa TSC Academy ambaye alipewa zawadi ya kipa bora na vifaa vyenye thanmani ya EURO 400 kutoka kwa kampuni ya kutengeneza vifaa vya magolikipa hapa Ujerumani.

 Pia wachezaji wengine ni, Miraji Madenge, Striker, Karlos Protus Centre back, Emily Mugeta left back, frank Sekule, Japhet Makalai na Saidi Juma.

Pamoja na kuwa kivutio kwa watu huku Ujerumani pia tumeweza kuitangaza nchi yetu na mpira wetu vizuri sana, kwani watoto na watu wazima wamekuwa wakitusupport sana, na kuchangia vitu mbalimbali vikiwemo viatu na mipira.

Lalini pia tumeweza kutembelea mashule mambalimbali na kifanya presentation juu ya mradi wetu wa michezo, ikiwa ni pamoja na kuwaonyesha video mambalimbali za maisha ya nyumbani kuhusiana na soka, elimu na maisha ya kila siku, baadhi ya shule tulizo tembelea ni mapoja na shule za primary, secondary na chekechea. Pia tuliwafundisha kupika ugali, kushona mipira na vitu vingine vingi.

Pia tulikaribishwa kwenye hafla zote na mameya wa miji tuliyotembelea na kucheza mashindania, Meya wa Mannheim, Meya wa Brackenheim, na meya wa Wurzbarg

Asante story na
Mutani Yangwe
Mkurugenzi TSC.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.