ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Wednesday, August 1, 2012

NAIBU WAZIRI WA ARDHI AHUDHURIA MAADHIMISHO YA 50 SHULE YA MSINGI NYAKAHOJA MWANZA

Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Goodluck Ole Medeye akishirikiana na ASKOFU Mkuu wa Kanisa Katoliki Jimbo Kuu la Mwanza Mhashamu Yuda Thaddaeus Ruwa'ichi kukata keki ya kusherehekea Jubilee hiyo ya shule ya msingi Nyakahoja kutimiza miaka 50


Mgeni rasmi Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Goodluck Ole Medeye (mwenye suti nyeusi katikati) pamoja na ASKOFU Mkuu wa Kanisa Katoliki Jimbo Kuu la Mwanza Mhashamu Yuda Thaddaeus Ruwa'ichi wakiongozwa kuingia viwanja vya maadhimisho kusherehekea Jubilee ya shule ya msingi Nyakahoja kutimiza miaka 50


Kwa upande wake Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Goodluck Ole Medeye ambaye alikuwa mgeni rasmi katika Jubilee hiyo ya shule ya msingi Nyakahoja kutimiza miaka 50 amewataka walimu kusitisha mgomo na kurejea kazini. Akisema kwamba walimu ni wazazi hivyo wanapaswa kuwa na utu, lakini pia wanapaswa kutambua kwamba mustakabali wa maisha ya wanafunzi yako mikononi mwao.


Masista na tabasamu la kutimiza miaka 50 Shule ya Msingi Nyakahoja.


Wageni na wazazi kwenye Jubilee hiyo.


Eneo mojawapo walioketi wanafunzi wa shule ya Msingi Nyakahoja.


Gwaride la wanafunzi wa Shule ya Msingi Nyakahoja wakitoa heshima wakati wa Wimbo wa Taifa la Tanzania.


Meza kuu na heshima za wimbo wa Taifa letu ndani ya Jubilee hiyo ya shule ya msingi Nyakahoja kutimiza miaka 50.


Gwaride la wanafunzi wa kike wa shule ya msingi Nyakahoja likipita heshima mbele ya halaiki ya watu waliohudhuria sherehe za kutimiza miaka 50 Shule ya msingi nyakahoja Mwanza. 


Hapa ni mwendo wa vipaji vya mmoja mmoja wanafunzi wa Prep Two.


Ni wanafunzi walioshiriki kama igizo flani hivi jukwaani kutoka kushoto ni Mwanafunzi, Dereva wa magari, Askari, Sister na Daktari kwenye pozi na flash ya blogu ya G. Sengo.


Kwaya ya Prep One.


Maigizo kijamii zaidi....


Ngoma za asili toka kwa wanafunzi wa shule ya msingi Nyakahoja zilihusishwa kwenye Maadhimisho ya 50.


Mc Mahiri mwenye sauti ya 'radi' Baba Paroko aliyesimamia zoezi hilo kikamilifu Mwanzo mwisho.


Ngoma iliyotia fora ndani ya maadhimisho hayo ya 50.


Mke wa Katibu Mkuu wa Chama cha CHADEMA Dk.Wilbroad Slaa, Josephine Slaa akimpa mkono ASKOFU Mkuu wa Kanisa Katoliki Jimbo Kuu la Mwanza Mhashamu Yuda Thaddaeus Ruwa'ichi  kwenye harambee ya kuchangia ujenzi wa shule ya sekondari wasichana ya nyakahoja, harambee iliyofanyika ndani ya Jubilee hiyo ya shule ya msingi Nyakahoja kusherehekea kutimiza miaka 50


Watoto wetu wakipata flash na blog yako.


Nikiwa na second bon wangu Cuthbert anayesoma shuleni hapo.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.