ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Tuesday, February 20, 2024

KATIBU WA CCM KIBAHA MJI AWAHIMIZA WANACHAMA KUGOMBEA UDIWANI KATA YA MSANGANI


VICTOR MASANGU,KIBAHA


Katibu wa Chama cha malinduzi (CCM) Wilaya ya Kibaha mjini Issack Kalleiya kuchangamkia fursa ya kujitokeza kwa wingi katika kuchukua fomu kwa ajili ya kugombea nafasi ya udiwani wa kata ya Msangani ambayo ipo wazi kwa sasa.


 Katibu huyo aliwahimiza wanachama wote ambao wana sifa za kugombea kujitokeza bila woga kwa lengo la kuweza kuziba nafasi hiyo ya diwani ambayo ipo wazi kutokana na aliyekuwa diwani wa kata hiyo kufariki dunia hivi karibuni.


Katibu  Kalleiya aliyasema hayo  wakati akizungumza na wajumbe wa Halmashauri Kuu ya Kata Msangani kuwa uchukuaji wa fomu ndani ya Chama utaanza tarehe 21/02/2024 hadi 23/02/2024 ambapo wanachama wote wenye sifa za kugombea watatakiwa kuchukua fomu na kurudisha ndani ya muda uliopangwa.

Amesema, Ofisi ya CCM Wilaya itakuwepo katika kuhakikisha kila mwanachama aliyechukua fomu anapata nafasi ya kuirudisha ili kusije kutokea malalamiko ya wagombea kukuta Ofisi za Kata zimefungwa.

Kalleiya alisema kwamba  zoezi hilo lonapaswa lifanyike kwa uweledi na kusisitika kuwa  hatopependa kusikia mwanachama yoyote ameshindwa kuchukua fomu yq Ugombea, bali kila mwenye sifa achukue ila maamuzi ya nani anafaa yatakuwa ni maamuzi ya Halmashauri Kuu ya Kata.

Pia, Katibu wa CCM amesisitiza kuhusu uundwaji wa Kamati za Ushindi katika kila Tawi na Mashina ili kuhakilisha Chama Cha Mapinduzi kinashinda nafasi hiyo kwa mara nyingine tena.
Akizungumzia suala la daftari la wapiga kura, Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Kibaha Mjini Ndg Mwl. Mwajuma Nyamka amesmea uchaguzi huu mdogo ni ww kujaza nafasi baada ya Diwani wa Kata ya Msangani kufariki ila kiutaratibu wale ambao walipiga kura katika Uchaguzi wa mwaka 2020 ndiyo wanapaswa kupiga kura.

Akifafanua zaidi, Mwenyekiti amesema kwa wale ambao wametimiza umri wa kupiga kura na hawakuwepo katika daftari la wapiga kura la mwaka 2020 hawataruhusiwa kushiriki Uchaguzi huu. 

Aidha, Kamati ya Siasa Wilaya iliweza kufanya ziara katika Matawi kila mmoja akiwa mlezi wa tawi na kusikiliza mawazo na ushauri wa wanachama ili kupata ufumbuzi wa changamoto zilizopo na kipi kifanyike na kuweza kupata ushindi wa kishindo.

Tume ya Uchaguzi nchini imetangaza tarehe ya Uchaguzi wa kujaza nafasi za Udiwani nchini ambapo Uchaguzi huo unatarajiwa kufanyika tarehe 20/03/2024.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.