NA VICTOR MASANGU, PWANI FEBRUARI 22
HALMASHAURI ya Kibaha mji mkoani Pwani katika kukuza sekta ya mchezo wa soka imetenga eneo lenye ukumbwa wa hekari 40 katika eneo la mintamba lengo ikiwa ni kujenga uwanja mkubwa wa kisasa ambao utatumika katika michuano mbali mbali ya kitaifa na kimataifa.
Kauli hiyo imetolewa na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Kibaha mji Mhe.Mussa Ndomba wakati wa halfa ya kufunga rasmi mashindano ya Kibafa Vijana Cup chini ya umri wa miaka 25 yaliyofanyika kwenye dimba la Mwendapole.
INSERT..1 TV MHE. MUSSA NDOMBA MWENYEKITI WA HALMASHAURI YA KIBAHA MJI.
Kwa upande wake Katibu wa mbunge wa Jimbo la Kibaha mjini Said Mbecha amebainisha kwamba wameweza kusapoti mashindano hayo kwa kuchangia zaidi ya shilingi milioni 6.
INSERT..2 TV SAID MBECHA KATIBU WA MBUNGE JIMBO LA KIBAHA MJINI
Kwa Upande wake Makamu mwenyekiti wa chama cha soka Mkoa wa Pwani (COREFA) Mohamed Lacha hakusita kumpongeza Mbunge wa jimbo la Kibaha mjini kwa kuamua kudhamini michuano hiyo kwa asilimia mia moja.
INSERT..3 TV MOHAMED MAKAMU MWENYEKITI WA CHAMA CHA SOKA MKOA WA PWANI(COREFA)
Naye Mratibu wa Mashindano hayo Walter Mwemezi amebainisha kwamba lengo lao kubwa ni kuinua na kukuza mchezo wa soka hasa kwa vijana
INSERT..4 TV WALTER MWEMEZI MENEJA WA MASHINDANO
Mashindano ya Kibafa Vijana Cup iliyodhaminiwa na Mbunge wa Jimbo la Kibaha mji Silivestry Koka imetamatika kwa timu ya Chestmocker kuwa mabingwa,na kuzawadiwa milioni moja,Umwerani mshindi wa pili na kupata laki tano na TP Pwani mshindi wa tatu na kupata seti ya jezi.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.