ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Monday, February 19, 2024

KOKA ATIMIZA AHADI YAKE AKABIDHI ZAWADI KWA MABINGWA MICHUANO YA KIBAFA VIJANA CUP


NA VICTOR MASANGU,KIBAHA 

MBUNGE wa Jimbo la Kibaha Mjini Silvestry Koka ametekeleza ahadi yake kwa vitendo kwa kutoa  fedha na vifaa vya michezo vyenye thamani ya shilingi milioni 1.7 kwa ajili ya kukabidhiwa  washindi watakashinda katika michuano ya  kombe la Kibafa  Vijana Cup wenye umri  chini ya miaka 25.

Michuano hiyo ya fainali ambayo ilikuwa inasubiliwa kwa hamu na shauku kubwa na mashabiki wa soka  inatarajiwa kulindima Februari 21  mwaka huu   kwenye uwanja wa Mwendapole mjini kibaha.

Akikabidhi zawadi hizo kwa niaba ya Mbunge katibu wa Mbunge wa Jimbo la Kibaha mjini  Method Mselewa wakati wa halfa fupi iliyofanyika katika ofisi za Mbunge na kuhudhuliwa na viongozi wa Kibafa na wadau wa soka.

Katibu Mselewa alibainisha  kwamba  wakati wa mashindano yananza Mbunge aliahidi kuwa mdhamini mkuu wa michuano hiyo na kutoa vifaa mbali mbali kwa ajili ya timu zishiriki.
Mselewa alibainisha kwamba ofisi ya mbunge imeweza kukabidhi zawadi mbali mbali ikiwemo fedha taslimu kiasi cha  shilingi milioni 1 kwa ajili ya timu itakayoibuka kuwa bingwa.

"Mbunge aliahidii kutoa zawadi kwa mshindi wa kwanza mpaka wa tatu na leo tumekabidhi zawadi hizo kwa viongozi wa Kibafa ambapo milioni moja kwa mshindi wa kwanza laki tano mshindi pili na mshindi  wa tatu zawadi ya jezi,"alisema Mselewa.

Aidha aliongeza kuwa mbunge aliamua kusapoti michuano hiyo kwa lengo la kuweza kukuza na kuibua vipaji kwa vijana wa jimbo lake ikiwa pia ni utekelezaji wa ilani ya chama.

Kwa upande wake Makamu Mwenyekiti wa Kibafa David Mramba amempongeza Kwa dhati kwa kuweza kusapoti mashindano hayo pamoja na kutoa jezi na vifaa Ili kufanikisha ligi hiyo ya vijana.

Pia alifafanua kwamba katika ligi hiyo Mbunge aliweza kutoa  jezi 16 pamoja na  mipira 20  kwa   timu zote 16 ambazo zimeshiriki katika michuano hiyo.

Naye meneja wa mashindano hayo Walter Mwemezi alisema alimpongeza Mbunge huyo kwa kuweza kufanikisha ahadi yake kwa vitendo kwa kutoa zawadi kwa timu zitakazoshinda.

Pia aliongeza kuwa mashindano hayo yameweza kupewa sapoti kubwa na mbunge kuanzia mwanzo na amekuwa mstari wa mbele katika kukuza sekta ya michezo.


Kivumbi cha fainali za  michuanoo hiyo ambayo ilizishirikisha timu 16 za Jimbo la la Kibaha mjini kinatarajiwa kufikia tamati yake Februari 21 mwaka huu katika viwanja vya mwendapole ambapo itazikutanishw timu ya Umwerani watamenyana na Chestmocker.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.