ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Thursday, August 19, 2010

MKENYA ALIYEMWUUZA ALBINO ATANDIKWA MVUA 17 NA FAINI JUU.

Baada ya kukiri kosa, Mahakama ya mkoa wa Mwanza nchini Tanzania imemhukumu Nathan Mutei (PIC-KUSHOTO) ambaye ni raia wa Kenya anayedaiwa kutaka kumwuuza albino kifungo cha miaka 17 gerezani na kutozwa faini ya zaidi ya shilingi milioni 80.

Polisi wamesema walimkamata Mutei alipojaribu kumwuuza mwenzake kutoka Kenya ambaye ni albino kwa kiwango cha sh milioni 400.

Mutei, mwenye umri wa miaka 28, alikamtwa nje kidogo ya mkoa wa Mwanza.

Katika harakati hizo za kumkamata, ziliyotangazwa rasmi siku ya Jumanne, polisi walijiweka katika nafasi ya wafanyabiashara wanaonunua viungo vya albino.


Kamanda polisi wa mkoa wa Mwanza, Simon Siro, amesema kuwa Bw Mutei alimlaghai Bw Mkwama (PIC-KULIA) mwenye umri wa miaka 20, kuwa atapata kazi Tanzania kama msaidizi wa dereva la lori.

Hapa nchini viungo vya maalbino vimekuwa vikitumiwa na waganga wa kienyeji kutengeneza dawa wanazowaambia wateja wao zitawasaidia kuwa matajiri au kuwa na afya njema.

Idadi kadhaa ya maalbino wameuawa, na mauaji hayo yameenea mpaka nchi jirani ya Burundi. Albino huyo, Robinson Mkwama, atasindikizwa kurudi nyumbani kwao nchini Kenya na ulinzi polisi.

MTUHUMIWA NGUVUNI.

Serikali ya Tanzania imeahidi kuwasaka wanaouza viungo vya albino, na wengi wamehukumiwa kifo kufuatia mauaji hayo.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.