.
. "Ole wao wale wanaotumia nafasi zao za umma na serikali, kuiba, kuhujumu uchumi, kupokea rushwa, maana salama yao ni kudra za Mwenyezi Mungu labda nisiwajue"
Hayo ni maneno aliyowahi kuyatamka hayati kaka na mzalendo wa taifa hili shujaa Moringe Sokoine, wakati akilihutubia kwenye mkutano kikao cha NEC mjini Dodoma 12/04/1984, wakati huo vita ya kupambana na suala la uzembe makazini, ulangunguzi, rushwa na biashara ya magendo, enzi hizo taifa lilikuwa la moto kila sehemu ilikuwa moto, mpaka #WALANGUZI wakamchukia...... lakini mpaka leo kauli yake inaishi, inatumika, inaamsha hali ya uzalendo na maadili ya taifa hasa wakati huu ambapo wanasiasa na serikali kwa ujumla wanaishi kinyume na misingi mikuu ya taifa hili, misingi mikuu ya chama chao na msingi mkuu wa uwajibikaji wa serikali, ingawa Rais #JPM kanyoosha watu si mchezo.
.
.
Leo tunakumbuka, kifo cha mpendwa wetu huyo kwa yale mazuri aliyoifanyia Tanganyika kwa ujumla wake, lakini pindi tunakumbuka kumbukumbu hii tujiulize je? Je viongozi wetu wanaishi kimatendo kama hayati Sokoine?
.
#Tafakari @jembefm
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.