ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Sunday, June 16, 2019

SIKU YA MTOTO WA AFRIKA NI MIAKA 43 SASA MACHOZI YASIYOFUTIKA KWA WANA WA AFRIKA KUSINI.

Safari ya Mwaka 2016 ya Mwanahabari/Blogger kutoka Jembe Fm Gsengo ilimfikisha hapa mbele ya kaburi la kijana Hector Pietersen.
Afrika Kusini inaadhimisha miaka 43 sasa tangu maandamano ya wanafunzi wa Soweto, walipopinga ubaguzi wa rangi katika elimu kwa kulazimishwa kusomeshwa kwa lugha ya Ki-Afrikaan.
Afrikaans ni lugha inayotumika huko Magharibi mwa Ujerumani na kabila dogo la nchi hiyo na ilitambulishwa hapa Afrika na makaburu kwa makusudi ya kuwachanganya waafrika wakibaki kuwa watumwa ikasambaa sehemu za Afrika ya kusini na Namibia.

Lugha hiyo haikuwa na msaada kwa wahitimu zaidi ya kuwachanganya pindi wanapo hitaji kwenda kwenye masomo ya juu au pindi wanapo ajiriwa wakashindwa kupenya kwenye nafasi za juu za uongozi na kubakia kuwa watumwa.

Mamia ya wanafunzi walifariki katika vurugu zilizojiri wakati serikali ya ukoloni ya wazungu makaburu ilipotumia nguvu kupita kiasi, kujaribu kuzima maandamano hayo.
Maandamano hayo yalikuwa kama mwanzo wa kuelekea hatua za kumalizwa kwa utawala wa makaburu wa Afrika Kusini.
Luis ni mwelekezi anayejitolea kwa watalii wanaodhuru eneo hili la kaburi la Hector Pieterson anasimuliwa kilichotokea. BOFYA PLAY KUMSIKILIZA 
(SAUTI ITAWAJIA HIVI PUNDE)
Ujumbe aliouandika mama wa kijana aliyebeba mwili wa kijana Hector Pieterson katika harakati za kumuokoa baada ya kupigwa risasi na polisi. Ujumbe unasomeka "Mbuyisa ni au alikuwa kijana wangu (kwa sababu alitoweka baada ya tukio hilo na hajulikani aliko mpaka sasa) akiendelea kusema ...... "Lakini si Shujaa. Kwenye utamaduni wetu kumbeba Hector siyo tukio la kishujaa, lilikuwa ni jukumu lake kama kaka. Kama angemuacha pale chini na mtu mwingine angemshuhudia akiuruka au kuukanyaga mwili wa marehemu Hector, asingestahili kuishi hapa"  ujumbe wa Ma'Makhubu.
Kila kilichopo hapa kina maana yake:-  Ukuta wa mawe yaliyopangwa ukimaanisha umoja wa watoto walioungana kwenye maandamano hayo kupinga ubaguzi, maji yanayotiririka yanaashiria machozi ya huzuni yaliyomwagika siku ya tukio toka kwa wazazi, watoto na taifa kwa ujumla, urefu unaopishana wa mawe unamaanisha umri wa watoto waliouawa, mianya katikati ya mawe inamaanisha taarifa zilizo potea au kufichwa hadi leo na kubaki bila ufafanuzi kama nani aliyemuua Pieterson na kadhalika, sakafu nyekundu ni damu iliyo mwagika, mawe ndani ya maji yanaashiria silaha pekee walizotumia watoto kujilinda dhidi ya polisi siku ya tukio.
Gsengo mbele ya picha ya mwili wa kijana Hector Pieterson uliobebwa na mwanafunzi mwenzake aitwaye Mbuyisa baada ya kupigwa risasi na polisi. Hii ndiyo picha iliyoibua hamasa na hasira kubwa na kuufanya ulimwengu kulaani ukatili uliokuwa ukiendelezwa na utawala wa makaburu enzi za ubaguzi wa rangi nchini Afrika Kusini.
a

Marehemu Hector Pieterson alizaliwa mnamo mwaka 1963 na June 1976 alikuwa ni mmoja kati ya mamia ya watoto waliouawa naye amewekwa kwenye historia kwani ni mmoja ya vijana wadogo waliouawa na makaburu na risasi ya kwanza ilimuua kijana huyo  akiwa na umri mdogo miaka 12 tu.
Pichani juu mwili wake ukiwa umebebwa na mwanafunzi mwenzake aitwaye Mbuyisa Makhubu baada ya kupigwa risasi huku dada yake akiwa naye anakimbia jirani kutafuta msaada.
Maji haya yanayotiririka mbele ya kaburi la Hector Pieterson yanaashiria machozi ya wazazi watoto na taifa juu ya tukio hilo la mauaji ya mamia ya watoto lililotokea mnamo tarehe 16 June 1976.

Jiwe hili lilitumika ngao kujikinga na risasi za mitutu ya bunduki za polisi kwenye maandamano ya watoto mnamo mwaka 1976.

a

Barabara hii ndiyo iliyo tumika kwa maandamano ya mwaka 1976 ikiwa ndiyo kiunganishi cha maeneo ya mji wa Soweto nchini Afrika Kusini.



Pembeni hatua chache kutoka eneo lilipo kaburi kuna Jumba hili la makumbusho la Hector Peterson, Humo ndani kunavielelezo vyote vya yale yaliyotokea kwa njia ya picha, video na baadhi ya mabaki ya nguo, silaha na baadhi ya nyezo walizotumia watoto hao kujikinga wakati wa vurugu zilizotokea zilizotumika kwenye tukio hilo lenye kumbukumbu yenye simanzi.


The Hector Pieterson Museum is a large museum located in Orlando West, Soweto, South Africa, two blocks away from where Hector Pieterson was shot and killed. Jumba hili lilipewa jina la marehemu kijana huyo kama heshima kwake.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.