Akizungumza na Waandishi wa habari Jijini Mwanza, Mkurugenzi Mtendaji wa F&G Promotions, Fabian Fanuel, alisema kuwa, Tamasha hilo la msisimko na laaina yake litahusisha kwaya, bendi na waimbaji binafsi kutoka maeneo mbalimbali ya Kanda ya Ziwa na nje ya kanda ya ziwa.Fanuel alizitaja baadhi ya Kwaya shiriki kuwa ni pamoja na Kwaya ya EAGT Msumbiji, Nyakato Moravian za Mwanza, Kwaya ya Mapambano kutoka Geita, AIC Ushirombo kutoka Ushirombo, Chipukizi ya Baptist Misungwi, T.A.G Vijana choir Geita, Ufunuo P.A.G choir, A.I.C Nyakato choir, Vijana Choir Nyakato, Tumaini Anglikan Igoma, Jerusalem choir, C.A.G Unguja, Imani Baptist choir Buhongwa, Revival Mission Band, Grace Wagana, Christina G. Vitta kuoka Kwimba, Tumaini KKKT Igoma choir, AIC Muungano choir, Mtakatifu Mkwasa RC choir Nyakato na Mwanza Gospel.
Fanuel alisema kuwa Tamasha hilo litafanyika sambamba na uzinduzi wa Kampuni hiyo F&G Promotions iliyojikita zaidi kwenye uandaaji wa matamasha ya aina mbalimbali kama vile maigizo, vichekesho pamoja na muziki wa aina mbalimbali kama vile, Muziki wa Injili, Muziki wa kizazi kipya, na Muziki wa Dansi.
Aidha, Fanuel aliwaomba wakazi wote wa Kanda ya Ziwa kujitokeza kwa wingi ili kushuhudia vipaji vya uimbaji kutoka ukanda wao, ambapo pia siku hiyo kampuni hiyo sambamba na kutambulisha wadau wake itatoa vyeti maalum kutambua mchango wa waimbaji, Redio mbalimbali pamoja na watumishi wa Mungu.
Tamasha la ‘Gospel Festival’ litakalokuwa likifanyika mara moja kwa mwaka, limelenga 'Kuamsha ari ya kiroho kwa watanzania kufanya kazi kwa imani na kutokata tamaa'
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment