ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Tuesday, December 20, 2011

WENJE AIWEZESHA SEKTA YA ELIMU NYAMAGANA

"Pamoja na Taifa Letu kuwa na uri mkubwa (miaka 50 ya Uhuru) sambamba na rasilimali tulizonazo, nchi hii inashika nafasi ya tatu kuwa ombaomba duniani, nchi ya kwanza ni Iraq ya pili ni Afriganstan nchi hizo zikiongoza kwasababu ya vita nchi ya tatu ni Tanzania"

Kama unakunywa kila siku pombe za shilingi elfu kumi na mtoto wako hana dawati anakaa chini shuleni basi juwa kuwa unafanya dhambi.

Madawati Mchango wa mbunge Ezekiel Wenje yatakayo zinufaisha shule mbalimbali za wilaya yake.

Madawati mchango wa mbunge wa Nyamagana Ezekiel Wenje yakitinga kusanyikoni.

"Kila baba mwema anapenda mtoto wake asome mahali pazuri, kama kungekuwa na shule mbinguni basi kila mwanaume angehangaika mwanae apate nafasi huko, lakini kwanini tusianze kuwatengenezea mazingira mazuri kuanzia hapa kwa kidogo tulichonacho?"

Umma uliofurika kumsikiliza mbunge Wenje

Wenje akipiga sahihi katika kadi za wanachama wapya walonunua kadi kwenye mkutano huo ambapo maelfu ya wanachama wapya walipatikana.

WENJE AKANA ONGEZEKO LA 'SITINGI ALAWANSI' asema tangu itajwe hajaiona kwenye akaunti yake. "Mimi Wenje sijalipwa na wala sijaiona posho iliyoongezeka inayoitwa sitting alowance, kimsingi kwa dhana tu ya kawaida ile posho ni siting alawansi, so hebu tujiulize utalipwaje kama haupo Dodoma, na Makinda alisema kama mnakumbuka maisha yamepanda Dodoma, sasa utalipwaje posho ukiwa Mwanza? na ile posho inatakiwa ukiwa pale bungeni ndiyo ulipwe, sasa mimi niliye huku jimboni mwangu Nyamagana nilipwe sitting alowance ya nini kwa lipi? Kama wanalipwa basi wanalipana wao kwa wao wanajuana"

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.