ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Thursday, January 6, 2022

MBUNGE KENYA AFUKUZWA KWA KUGAWA PEREMENDE BUNGENI.

 
Mbunge wa Kenya siku ya Jumatano alifurushwa kikaoni kwa siku moja baada ya kupatikana akifawanya peremende kwa wenzake wakati mjadala ulipokuwa ukiendelea.


Fatuma Gedi alisema "viwango vya sukari vilikuwa vimeshuka" baada ya kushiriki kikao kirefu.


Alikuwa ametuhumiwa na mbunge mwenzake Ndindi Nyoro kwamba alikuwa akigawanya pesa ndani ya ukimbi wa bunge.


Bw Nyoro aliombwa kuthibitisha madai yake ya hongo na kuzuiliwa kuhudhuria vikao kwa siku mbili baada ya kukosa kufanya hivyo.


Bi Gedi alizuiliwa kuhudhuria kikao kimoja kwa kosa la kugawanya bungeni.


Wabunge waliidhinisha marekebisho kadhaa katika mswada wa vyama vya siasa kabla ya uchaguzi mkuu wa mwaka huu


Tazama kilichotokea wakati wabunge walipotoa madai ya hongo:

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.