ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Thursday, January 6, 2022

UJENZI BARABARA NJIA NNE KUANZIA MBEYA.

 


Msongamano wa  magari katika barabara kuu ya Tanzania na Zambia (Tanzam) umetafutiwa ufumbuzi kufuatia kuanza kwa utekelezaji wa ujenzi wa barabara za njia nne kutoka Igawa Wilayani Mbarali mpaka Mji wa Tunduma Mkoa wa Songwe.


Akizungumza na Mwananchi leo Alhamisi Januari 6, 2021 Naibu Spika na Mbunge wa Jimbo la Mbeya, Dk Tulia Ackson amesema kuwa  kwa sasa tayari upembuzi yakinifu umeshafanywa kinachosubiria ni utekelezaji wa mradi wa barabara njia nne katika barabara kuu ya Tanzania na Zambia.


''Tayari fedha za mradi tumepata kwa ufadhili wa benki ya dunia na miundombinu hiyo ikikamilila itaondoa hadha ya msongamano wa magari na kuchochea shughuli za kiuchumi''amesema.


Dk Tulia amesema kuwa Serikali ya awamu ya sita imewekeza katika miradi mbalimbali ambapo katika Jiji hilo wameweza kuboresha miundombinu korofi ambapo baada ya kupokea Sh2 bilioni.


''Wakati mradi huo wa njia nne ukiwa unaanza utekelezaji na barabara za jiji zimeboreshwa katika maeneo ambayo yalikuwa yakisababisha msongamano wa magari kwa kuboresha barabara za michepuko ''amesema.


Dereva wa magari ya mizigo, Salim Ally amesema kuwa endapo Serikali ikaharakisha ujenzi wa miundombinu ya barabara nne itakuwa na mchango mkubwa katika shughuli za kiuchumi na kwamba msongamo wa magari umekuwa changamoto kubwa kwao.


'' Kwa sisi Madereva wa masafa marefu foleni kwetu ni changamoto kwani tunapaswa kuwahi Tunduma kupanga foleni kwa ajili ya kulipia vibali mbalimbali mpakani sasa unakuta kuna wakati tunatumia muda mwingi kukaa njiani'amesema.


Ameishauri Serikali kupitia Wizara husika kuharakisha mradi huo ili uweze kuleta tija kwao na taifa kwa ujumla kwani Sekta ya usafirishaji imekuwa na mchango mkubwa katika kuchangia pato la Taifa.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.