Na Fredy Mgunda,Iringa.
MAMLAKA ya Dawa na Vifaa Tiba (TMDA) kuwajengea
uwezo wataalamu wa ukaguzi wa dawa na vifaa tiba katika Halmashauri zote za
Mkoa wa Iringa kwa lengo la kuboresha ufanisi wa kazi wawapo kazini ili kulinda
afya za watumiaji wad awa na vifaa tiba.
Akizungumza wakati wa kufungua
mafunzo hayo kaimu katibu tawala mkoa wa Iringa,Elias luvanda alisema kuwa ni
kielelezo tosha kuwa wakaguzi ngazi ya Halmashauri mnathamini mchango wa TMDA
katika kuwapa elimu kuhusu namna bora ya kutekeleza majukumu na kulinda Afya za wananchi ili waweze kushiriki
kikamilifu katika ujenzi wa taifa letu la Tanzania.
Luvanda alisema kuwa Mamlaka ya
Dawa na Vifaa Tiba (TMDA) ni taasisi iliyo chini ya Wizara ya Afya, yenye
jukumu la kudhibiti ubora, usalama na ufanisi wa Dawa, Vifaa Tiba na
Vitendanishi na Taasisi hiyo imeundwa chini ya sheria ya Dawa na Vifaa Tiba
sura 219.
Alisema
kuwa majukumu yanayofanywa na TMDA na yale yaliyokasimishwa kwenu, lengo lake
ni lilelile la kulinda afya ya jamii kwa kuzuia athari zinazoweza kujitokeza
kutokana na matumizi ya dawa, vifaa tiba na vitendanishi.
“Kwa
kutambua jukumu zito la TMDA, Serikali iliona ni vema kukasimu baadhi ya
madaraka na majukumu yao kwa Halmashauri kwa lengo la kusogeza karibu na
wananchi huduma za udhibiti wa ubora na usalama wa dawa, vifaa tiba na
vitendanishi”alisema Luvanda
Luvanda aliwataka watendaji wote
kufanya kazi kwa kutoa taarifa zilizo sahihi kwa wakati unatakiwa ili
kurahisisha utendaji wa taasisi hiyo hivyo Mwongozo wa Kukasimu Madaraka na
Majukumu umebainisha wazi kuwa taarifa za utendaji kazi za robo mwaka na
taarifa za ufuatiliaji na tathmini ya utekelezaji wa kazi za udhibiti wa ubora,
usalama na ufanisi wa bidhaa zinazodhibitiwa katika soko zinatakiwa kuandaliwa
na kutumwa TMDA kupitia viongozi wa ngazi ya Halmashauri.
“Ni mategemeo yangu kwamba mafunzo haya yatatoa
maelekezo ya namna ya kuboresha utendaji kazi wenu, na kuondoa changamoto
zinazojitokeza mara kwa mara kuwa, wakaguzi wa Halmashauri wanatumia nguvu
nyingi nyakati za kaguzi ambazo husababishwa na kutokutoa elimu kwa wateja
(wafanyabiashara) Hivyo kukinzana na utaratibu wa ukaguzi wa TMDA ambao
umejikita zaidi katika kuelimisha na kuwezesha” alisema Luvanda.
Alimalizia kwa kusema kuwa Ofisi
ya Mkuu wa Mkoa itafanya ufuatiliaji wa utekelezaji wa maagizo na makubaliano
yatakayowekwa ili kuhakikisha wananchi wanahakikishiwa upatikanaji wa bidhaa
bora na salama.
Kwa upande wake Meneja wa Mamlaka
ya Dawa na Vifaa Tiba (TMDA) kanda ya kati
Sonia Mkumbwa alisema kuwa lengo la mafunzo hayo ni kuwaongezea ujuzi wakaguzi
ili waweze kufanya kazi ya ukaguzi kwa kuzingatia sheria.
Mkubwa alisema kuwa wakaguzi
watatekeleza kazi zao kwa kuzingatia sheria, kanuni na miongozo kama zilivyotolewa
na TMDA kama vile Kufanya ukaguzi wa maeneo yanayohusika na utunzaji,
uuzaji na usambazaji wa dawa, vifaa tiba na vitendanishi, Kufanya ufuatiliaji
na kutoa taarifa za ubora na usalama wa dawa, vifaa tiba na vitendanishi katika
soko.
Aliongeza kuwa wakaguzi watatakiwa kuchukua sampuli za bidhaa
zinazodhibitiwa kwa ajili ya uchunguzi wa kimaabara pale inapohitajika na kufanya ufuatiliaji wa madhara/matukio yanayohisiwa
kusababishwa na matumizi ya dawa, vifaa tiba na vitendanishi.
Mkumbwa
alisema kuwa wakaguzi wanatakiwa kufanya uhakiki wa bidhaa zisizofaa kwa
matumizi kabla ya uteketezaji kwa kujaza fomu ya uhakiki (Kiambatisho Na.7)
baada ya mawasiliano na Ofisi ya Kanda ya TMDA na kusimamia zoezi la kuteketeza
bidhaa ambazo hazifai kwa matumizi baada ya uhakiki na kisha kujaza fomu ya
uteketezaji (Kiambatisho Na. 8) na kuiwasilisha ofisi ya Kanda ya TMDA kwa
ajili ya kuandaa cheti cha uteketezaji.
Alimazia kwa kuwasema kuwa kila
Halmashauri itaandaa na kuwasilisha taarifa za utendaji kazi kwenye Ofisi za
TMDA za Kanda na kuwasilisha nakala kwa
Katibu Tawala wa Mkoa ambazo ni taarifa ya utendaji ya robo
mwaka na taarifa
ya ufuatiliaji na tathmini ya utekelezaji wa kazi za udhibiti wa ubora, usalama
na ufanisi wa bidhaa katika soko.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.