NA ALBERT G. SENGO/UKEREWE
Halmashauri ya wilaya ya ukerewe mkoani mwanza imefanikiwa kuokoa shilingi millioni 74 kwenye mradi wa ujenzi wa Jengo la wagonjwa wanaohitaji uangalizi maalum(ICU)katika Hospitali ya BWISYA iliyopo kwenye kisiwa cha Ukara wilayani humo. Mganga mfawidhi wa hospitali hiyo DOKTA ALEX SIBONA amesema kuwa fedha hizo ni kati ya shilingi millioni 251 zilizotolewa na serikali kuu kwa ajili ya kugharamia utekelezaji wa mradi huo. Ujenzi wa mradi wa ICU katika hospitali ya BWISYA umefikia hatua za mwisho kukamilika ambapo Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya ukerewe EMMANUEL SHELEMBI amewaasa wananchi kuendelea kuunga mkono Jitihada za serikali ili kuchochea maendeleo ya kiuchumi na kijamii. Wilaya ya ukerewe kwa sasa haina huduma ya ICU na Hospitali ya BWISYA inatarajiwa kuwa ya kwanza kutoa huduma hiyo.Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.