ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Friday, December 16, 2022

MKENYA AISHIYE MAREKANI AKUTWA AMEFARIKI CHUMBANI KWAKE.


 Usiku wa Jumamosi ya Desemba 10, Kevin Odero alikuwa nyumbani kwa wazazi wake huko Connecticut, Marekani, na dada yake mdogo alipokata roho ghafla. Kulingana na dadake, mwili wa Kevin tayari ulikuwa umebadilika na kuwa rangi ya zambarau polisi walipofika. 

Wakati huo babake kijana huyo mwenye umri wa miaka 20 alikuwa amesafiri hadi Kenya na kuwaacha, bila kujua kwamba mauti yangelimfika mwanawe mpendwa. 

Dadake Kevin Elizabeth Odero alimwambia Hillary Lisimba wa TUKO.co.ke kwmaba dada yao aligundua mwili wa kaka yao ingawaje kwa kuchelewa. 

Kwa mujibu wake, mwili wa kijana huyo ulikuwa tayari umegeuka zambarau na juhudi za kupigia simu ya 911 ya huduma za dharura kuja kumkimbiza hospitalini hazikuzaa matunda. 

 “Walijaribu kumuamsha lakini maafisa wa afya walithibitisha kuwa tayari alikuwa amefarik dunia, ndiposa polisi walipochukua maiti ili kufanya uchunguzi,” alieleza. 

Elizabeth alifichua kuwa marehemu alikuwa na umri wa miaka 20, alizaliwa na kukulia Nairobi lakini alijiunga na familia yake Marekani mnamo 2020. 

Wakati wa kifo chake, alikuwa amemaliza tu diploma yake ya shule ya upili na alikuwa akifanya kazi ya muda huko Amazon. 

Mojawapo ya mipango ya Kevin kwa mwaka ujao ilikuwa kujiunga na chuo cha ufundi mwezi Januari na kuendelea na kozi ya ufundi wa mabomba. 

"Mwili wake ulichukuliwa na polisi jana na kwa sasa umelazwa katika makafani moja huko Massachusetts," alisema Elizabeth. 

Familia yake kwa sasa inajaribu kuchangisha dola 18,000 (KSh 2.2 milioni) ili kuwezesha mwili wake kurejeshwa nchini Kenya kwa mazishi. 

 Katika michakato mtandaoni iliyolenga kusaidia kuchangisha fedha, Kevin alisifiwa kama "mwana mpendwa wa Joseph Odero na kaka wa Virginia wa New Haven Connecticut na Adrian Amani."

 "Tafadhali mkumbuke Joseph na binti yake katika maombi na ujisikie huru kuwaambia marafiki wengine na kuwaongeza kwenye kikundi," sehemu ya chapisho hilo ilisema. 

Elizabeth alifichua kwamba familia hiyo itaandaa misa ya wafu Desemba 23 kisha mwili utasafirishwa hadi nchini Kenya kwa mazishi. 

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.