Mkuu wa wilaya ya Nachingwea Mohamed Hassan Moyo akiongea na wananchi kuacha mara moja tabia ya kuwawekea vijiti watoto wao
Na Fredy Mgunda, Iringa.
MKUU wa wilaya ya Nachingwea Mohamed Hassan Moyo amewataka wanawake kuacha tabia ya kuwawekea vijiti vya uzazi wa mpango watoto mwenye umri wa chini ya miaka 18 kufanya hivyo sawa na ukatili wa kijinsia.
Akizungumza wakati mkutano wa hadhara katika Kijiji cha Litula, Moyo aliwataka wanawake kuacha mara moja tabia kuwawekea vijiti watoto wadogo kwa kuwa hawajui madhara yake.
Moyo alisema tabia ya kuwawekea vijiti watoto wakiwa na umri mdogo kutasababisha waanze kufanya mapenzi katika umri huo bila kuwa na woga wowote ule.
Alisema kuwa ataanzisha msako maalumu kwa kila shule ili kubaini wanafunzi wangapi wamewekewa vijiti na ni nani kawawekea vijiti hivyo na hatua kali za kisheria zitachukuliwa.
Aidha Moyo aliwataka wazazi wa wilaya hiyo kuwafundisha watoto amaadili mema ambayo yatawasaidia watoto walelewe katika misingi inavyotakiwa.
Moyo alimazia kwa kusema kuwa kuwawekea vijiti watoto kunawakinga na mimba pekee yake vipi kuhusu magonjwa mengine kama vile ukimwi,kisonono,na mengine yanayotokana na ngono zembe
Kwa upande wao wazazi wa watoto hao walikiri kufanya jambo hilo la kuwawekea vijiti vya uzazi watoto wao ili kuwaepusha na mimba za utotoni ambazo zimekuwa zikikatisha ndoto za maisha yao mapema.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.