Na Fredy Mgunda, Iringa.
Mjumbe wa Kamati ya Siasa ya Mkoa wa Iringa Dkt Tumaini Msowoya amewaasa wasichana wa kidato cha sita kuwekeza katika bidii, utii na kumcha Mungu kama ngao yao ya mafanikio.
Dkt Msowoya alikuwa mgeni rasmi kwenye mahafari ya kidini ya TYSS, kwa wanafunzi wa kike wa kidato cha sita katika Shule ya Sekondari ya Mbalamaziwa, Wilayani Mufindi, Mkoani Iringa.
"Hata ukifaulu kwa alama za juu sana kama sio mtii, humchi Mungu bidii yako ni bure tu," amesema.
Mjumbe huyo wa Kamati ya Siasa ya Mkoa wa Iringa pia aliwapongeza walimu na viongozi wa Kanisa la Roman Katholiki kwa kuwafundisha wanafunzi hao katika msingi wa maadili kiasi cha kuwafanya wajitambue.
Awali, Paroko wa Patokia ya Nyakipamba, Padre Kizito Fungo aliwaasa wahitimu hao kumtanguliza Mungu katika kila jambo.
Nae Makam Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Mbaramaziwa, Sister Revina Kilai amesema wanafunzi hao wameandaliwa vizuri tayari kwa kukabiliana na mitihani.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.