WAZIRI wa mambo ya ndani Kangi Lugola na mkuu wa jeshi la polisi nchini Simon Sirro wameombwa kutoa maagizo kwa jeshi la polisi nchini kutambua uwepo wa waandishi wa habari wanapokuwa wanatekeleza majukumu yao kutokana na kukithiri kwa vitendo vya jeshi hilo kuwakamata waandishi wa habari pindi wanapokuwa wakitekeleza majukumu yao ya kikazi.
Ombi hilo limetolewa jijini Mwanza na Chama cha waandishi wa habari wa kupiga vita matumizi ya dawa za kulevya na uhalifu Tanzania [OJADACT] kwa kushirikiana na klabu ya waandishi wa habari mkoa wa Mwanza [MPC] kufuatia tukio la kukamatwa waandishi wawili wa habari wakati wakitekeleza majukumu yao katika kituo cha polisi Nyakato mkoani Mwanza.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.