Mkuu wa Mkoa wa Songwe Brig. Jen. (Mst) Nicodemus E. Mwangela akitoa salamu za pole kwa niaba ya Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli kwa ndugu, jamaa na marafiki wa wafiwa, kufuatia ajali ya gari iliyosababisha vifo 19.
Ndugu, jamaa na marafiki wa wafiwa, kufuatia ajali ya gari iliyosababisha vifo 19 wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Songwe Brig. Jen. (Mst) Nicodemus E. Mwangela akitoa salamu za pole.
Mkuu wa Mkoa wa Songwe Brig. Jen. (Mst) Nicodemus E. Mwangela akikagua majeneza kabla hayajakabidhiwa kwa wafiwa, kufuatia ajali ya gari iliyosababisha vifo 19.
Sehemu ya Majeneza 19 yaliyotolewa na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Songwe kufuatia ajali iliyohusisha magari matatu, mkoa pia umewezesha usafiri wa miili ya marehemu hao.
MKUU wa Mkoa wa
Songwe Brig. Jen. (Mst) Nicodemus E. Mwangela anatoa salamu za pole kwa niaba ya
Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli kwa ndugu,
jamaa na marafiki wa wafiwa, kufuatia ajali ya gari iliyosababisha vifo 19
ikiwa wanaume ni 15 na wanawake wanne.
Brig. Jen. (Mst)
Mwangela amesema kutokana na ajali hiyo iliyotokea usiku eneo la Senjele
Wilayani Mbozi ikihusisha magari matatu yaliyokuwa yakielekea Mbeya kugongana,
serikali Mkoani Songwe imetoa majeneza 19 pamoja na usafiri kwa ajili ya
kuhifadhi miili ya marehemu.
“Rais Magufuli
amenituma niwape pole na ametuelekeza kama Mkoa kusimamia Mamlaka za Usalama
barabarani kufanya uchunguzi na hatua zinazo stahili kuchukuliwa, pia
ameelekeza tujipange vizuri kukabiliana na matukio ya ajali za barabarani”, amesema
Brig. Jen. (Mst) Mwangela.
Brig. Jen. (Mst)
Mwangela amesema chanzo cha ajali hiyo kimetokana na gari la abiria aina ya
coaster kugongwa na gari la mizigo lililokuwa nyuma yake kisha coaster kugonga
gari la mizigo lililo kuwa mbele yake na kupelekea gari la abiria kubanwa
katikati ya magari mawili ya mizigo.
Aidha ameliagiza
Jeshi la Polisi Mkoa wa Songwe, kuweka utaratibu maalumu wa magari kupita kwa
kupokezana katika maeneo yote yenye miteremko mikali, kuwepo ukaguzi wa magari
kabla hayajaanza kushuka au kupanda mlima pamoja na kuweka ulinzi wa maeneo hayo.
“Mungu ametupa akili
za kufanya kazi na akili hizi tuzitumie kuzuia ajali ndani ya Mkoa wa Songwe,
hivyo nawasihi watumiaji wote wa vyombo vya moto kuhakikisha wanafuata sheria
za usalama barabarani ili kuweza kuepuka ajali kama hizi”, amesisitiza Brig.
Jen. (Mst) Mwangela.
Mapema jana Brig.
Jen. (Mst) Mwangela amefika katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Songwe ambapo
miili ya marehemu ilikuwa imehifadhiwa ili kuwafariji wafiwa waliofika kutambua
miili ya ndugu zao.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.