NA
ALBERT G. SENGO:MWANZA
Ikitumia Vyema uwanja
wake wa nyumbani Pamba Fc ya Mwanza leo imeanza vyema mchezo wake wa
kwanza kundi C ya Ligi ya soka Daraja la kwanza ya Tanzania bara kwa kuichapa
Polisi Mara kwa mabao 3-2.
Magoli ya Pamba
yalifungwa na Mathayo William dakika ya 3, Shahban Makoba dakika ya 61 na
Mashaka Kiumba dakika ya 70.
Upande wa timu ya Polisi
Mara magoli yake yalifungwa na Kaichi Kaichi kwenye dakika ya 4, na Athumani
Matutu aliyefunga bao la pili dakika ya 90.
Makocha wa timu zote mbili walipata fursa kuzungumza na Sports Xtra juu hali ya mchezo na nini matarajio kwa mechi zinazofuata za kundi C, Ligi soka Daraja la kwanza Tanzania bara.
Msikilize Wa kwanza ni kocha wa timu ya Pamba ya jijini Mwanza Ibrahim Mulumba..
Naye kocha wa Polisi mara Hafidh Salim amewaumu wachezaji wake kuingiwa kitete na mchezo huo wakiacha maelekezo yake na kucheza kila mmoja kimpango wake...
MWISHO
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.