|
Askari polisi jijini Mwanza wakiwa na wakaguzi kutoka FCC kuhakiki ubora wa bidhaa ya nyembe zinazotengenezwa na kampuni ya Super Max. |
BIDHAA zinazotengenezwa na Kampuni ya Super Max ya nchini Dubai imegudua bidhaa zake za Nyembe kuchakachuliwa na kuuzwa katika baadhi ya maduka ya jumla katika mikoa mbalimbali hapa nchini huku Jijini Mwanza maduka kumi yakikutwa yakiuza bidhaa feki za wembe wa Super Max.
Msako wa kushitukiza kutoka kwa maafisa wa Taasisi ya Fear Competition Commission (FCC) na maasifa watatu wa Kampuni ya Super Max wakiwa na mwanasheria wao sanjari na askari polisi walifanya msako huo na kukuta bidha hizo zisizo na ubora zikiuzwa huku zikiwa na jina la Kampuni ya Super Max ambapo pia nembo ikiwa tofauti kabisa na ile ya bidhaa zenye ubora kutoka kampuni ya super max ya nchini India.
|
Mmoja wa wafanyabiashara katika mtaa wa Liberty baada ya kukutwa akiuza bidhaa feki na orijino, (Super Max yenye rangi ya njano na kijani ndiyo orijino na ile ya blue ni magumashi aka feki) |
Zoezi hilo lilionekana kuwa na mafanikio makubwa pia liliwapa changamoto baadhi ya wafanyabiashara kuanza kuzikagua bidha wanazokuwa wananunua na kuziuza kwa wateja wao endapo zina nembo ya shirika la viwango nchini (TBS) ili kuepuka usumbufu na madhala kwa wateja wao wanaovitu vitu hivyo.
|
Mmoja kati ya maafisa wa FCC walioongoza zoezi hilo akitoa wito kwa wafanya biashara. |
Afisa wa Kampuni ya Super Max Bw.Emmanuel Shija alieleza kuwa kufanyika kwa msako huo kunatokana na kuwepo kwa malalamiko kutoka kwa baadhi ya wateja wao wakidai kuwa bidhaa za super max zimekuwa hazina ubora hususani wembe ambazo zinapotumiwa na wateja wao hazina makali na zimekuwa zikikatika hali ambayo iliwalazimu kufanya uchunguzi na kukungundua kuwepo kwa bidhaa feki sokoni zenye nembo ya kampuni hiyo.
“Tumekuwa tukiwaelimisha wateja wetu ambao ni wafanyabiashara wa bidhaa zetu kuwa makini na bidhaa ambazo huingizwa nchini kwa njia za panya na hata wakati mwingine kubadilishiwa makasha huku yakiwa hayana hata mhuri wa TBS ili kuepuka kuwauzia wananchi kwa kutambua kuwa bidhaa hizo hazina ubora unaotakiwa huku pia vikiwa havijatengenezwa na kampuni yetu”alisema.
|
Mzigo wa nyembe feki uliokutwa kwenye baadhi ya maduka mtaa wa Liberty jijini Mwanza. |
Naye Afisa mdhibiti wa vifaa bandia toka FCC Bw.Emmanuel Ndyetabula alieleza kuwa wamekuwa wakifanya ukaguzi wa mara kwa mara hasa pale wanapotaarifiwa kuwepo bidhaa bandia sokoni pamoja na kufanya ukaguzi wa kawaida katika maeneo mbalimbali nchini ikiwemo Mkoa wa Mwanza na Wilaya zake bila kujali kuwa bidhaa hizo zimegaramiwa fedha nyingi na wafanyabiashara hao.
|
Bidhaa za Super Max zenye ubora na orijino ndiyo hizi ambapo kuna Green na Blue Diamond. |
“Lengo kubwa ni kuhakikisha bidhaa zote zinazoingizwa sokoni na kutumiwa na wateja ni zile tu zenye ubora unaotakiwa na si vinginevyo ili kuepuka madhala kwa watumiaji pamoja na Taifa kuwa na bidhaa ambazo hazina ubora na zisizo faa kwenye matumizi ya binadamu mbali na kukamata bidha hizo wanaokutwa nazo pia tumekuwa tukiwalipisha faini ili kusaidia kutoendelea kuzifanyia biashara bidhaa hizo kwa vile watakuwa wanatambua hasara watakazopata baada ya kukutwa nazo”alisisitiza.
|
Hizi ni bidhaa feki kuwa wangalifu. |
Bw.Ndyetabula
alisema kuwa baada ya maafisa wa Kampuni ya Super max kuleta malalamiko yake
kwetu na tulipo hoji iwapo anao ushahidi wa kutosha walitueleza kuwa wamefanya
uchunguzi wa kina na kugundua kuwa bidhaa nyingi za kampuni hiyo
zimechakachuliwa na zinauzwa kwa wingi katika maduka mengi ya Jijini Mwanza
ndiyo hasa bado yalikuwa yanauza bidhaa hizo feki.
|
Msako ukiendelea kwa maduka ya Mwanza. |
Kwa
upande wake Meneja masoko na mauzo wa Kampuni ya Super Max Bw.Kartesh Patil
kutoka nchini Dubai alisema kuwa soko kubwa la usambazaji wa bidhaa hizo lina
ofisi zake nchini humo hivyo kuja kufanya ukaguzi wa kugundulika kuwa bidhaa
hizo zimechakachuliwa na kuingizwa sokoni kwa lengo la kuharibu jina la kampuni
limewagarimu kuja kupigania haki yao ya kibiashara ili bidhaa zao ziendelee
kuwepo sokoni lakini kwa ubora unaotakiwa na kuendelea kutoa elimu na mifano ya
bidha zao zenye ubora na nembo halisi ya kampuni hiyo.
|
Super Max yenye rangi ya njano na kijani ndiyo orijino na ile ya blue ni magumashi aka feki. |
Bw.Patil
ametoa wito kwa wafanyabiashara kuendelea kuuza bidhaa za kampuni yake zilizo
na ubora na zenye nembo halisi badala ya kukubali kuingizwa mkenge na kutumia
bidhaa zenye nembo ambayo haifanani kabisa na ile ya kampuni kuepuka usumbufu
kama walioupata wa kuchukuliwa bidhaa zao hizo na kutozwa faini hali
itakayoweza kuwayumbisha kibiashara kutokana na garama kubwa wanazozitumia.
"Haya-hayaaaa.. Kazi kwenu wanyoaji na wanyolewaji, wito kuweni makini.... Feki zinamadhara zaweza kukupa tetenasi....Tehe-teh!!"
Tupe maoni yako
Very nice coverage. Congrats.
ReplyDelete