Ingawa kwa sasa lile wimbi la mauaji yenye nia ya kuchukuwa viungo vya miili ya albino limedhibitiwa lakini bado ndugu zetu hawa wanakabiliana na tatizo jingine la unyanyapaa, suala ambalo limekuwa sugu na kuwaathiri wengi kulingana na maeneo wanayoishi watu hao.
Unyanyapaa umekuwa na viwango vyake na uko kwenye madaraja.. kwani kwa maeneo ya mijini suala la unyanyapaa limedhibitiwa kupitia usambaaji wa elimu itolewayo kupitia radio mbalimbali, majarida, makongamano na mitandao ya kijamii tofauti na ngazi ya wilayani na vijijini ambako mijadala imekuwa michache na upashaji habari hauna nyenzo za kuwafikia wananchi. |
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.