Mwanafunzi wa kidato cha kwanza katika shule ya sekondari Old Shinyanga Rashid Mashaka miaka 14 amefariki dunia baada ya nyumba aliyokuwa amelala kuungua moto.
Tukio hilo limetokea usiku wa kuamkia Machi 10 majira ya saa 6 usiku katika kitongoji cha Senyenge kata ya Old Shinyanga baada ya shoti ya umeme kutokea katika nyumba hiyo kisha moto kuwaka na kuunguza vitu mbalimbali wakati kijana huyo akiwa amelala ndani.
Mama mzazi wa mtoto huyo Fatuma Rajab ambaye hakuwepo nyumbani wakati wa tukio hilo amesema mvua zilizonyesha jana zilisababisha umeme kukatika na uliporejea majira hayo ndipo shoti hiyo ilipotokea kisha nyumba yake kushika moto.
Kamanda wa kikosi cha zimamoto na uokoaji wilaya ya Shinyanga Inspekta Stanley Luhwago amesema kuwa chanzo cha moto huo ni shoti ya umeme iliyoanzia kwenye mita ya nyumba hiyo.
Kijana huyo alikuwa akisoma kidato cha kwanza shule ya sekondari Old Shinyanga.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.