Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP Simon Sirro, amefanya mabadiliko ya Makamanda wa Jeshi la Polisi katika mikoa miwili ya Kagera na Rukwa.
Taarifa ya Jeshi la Polisi imeeleza kuwa mabadiliko hayo ni kupisha uchunguzi wa kauli za aliyekuwa RPC wa Kagera ACP Wankyo Nyigesa alizozitoa wakati anaaga baada ya kuhamishwa kutoka Pwani kwenda Kagera.
Katika mabadiliko hayo, Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP Simon Sirro amemhamisha aliyekuwa RPC mkoa wa Rukwa William Mwampagale kwenda kuwa RPC mkoa wa Kagera, kuchukua nafasi ya aliyekuwa RPC wa mkoa huo ACP Wankyo Nyigesa ambaye amehamishiwa Makao Makuu ya Polisi Dodoma.
Aidha IGP Simon Sirro amempandisha aliyekuwa Afisa Mnadhimu wa mkoa wa Rukwa ACP Theopista Mallya kuwa RPC wa mkoa huo, akichukua nafasi ya ACP William Mwampagale ambaye amekwenda kuwa RPC mkoa wa Kagera.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.