Wizara ya Ulinzi ya Marekani metangaza kutenga kiasi cha kitita cha dola milioni 300 ukiwa "msaada wa usalama" kwa Ukraine ili kuimarisha uwezo wa ulinzi wa nchi hiyo, kikiwa ni nyongeza ya kiasi kingine cha dola bilioni 1.6 ambacho taifa hilo lilikiahidi kukitoa tangu Urusi ilipoanza uvamizi Februari.
Taarifa ya msemaji wa wizara hiyo John Kirby inasema hatua hiyo inaonesha usisitizwaji wa dhamira isiyotetereka ya Marekani kwa taifa la Ukraine katika kulinda uhuru wake wa kimipaka baada ya kuvamiwa.
Jumatano iliyopita Rais Joe Biden wa Marekani na yule wa Ukraine, Volodymyr Zelensky walijadiliana juu ya nyongeza ya msaada wa ziada katika kulisaidia jeshi la Ukraine.
Taarifa hiyo ilitolewa na Ikulu la Marekani baada ya mazungumzo hayo kwa njia ya simu.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.