MBUNGE wa Vitimaalum Mkoa wa Mwanza, Maria Hewa
(CCM), ameawataka wananchi wa Kata ya Mahina kutowapigia kura wagombea nafasi ya
wenyeviti wa Mitaa na wajumbe wao wa vyama ambavyo wamekuwa wakiwatukana matusi
na kuwadhalilisha wagombea wenzao jukwaani.
Akizungumza kwenye mkutano wa hadhara wa jana,
wakati wa kuwanadi wagombea wa nafasi za wenyeviti wa mitaa 20kupiutia Chama
chake, alisema kuwa wakati huu wa kampeni kumeibuka baadhi ya viongozi ambao
wamekuwa wakiwatukana hadharani wagombea wenzao na kusema uongo jambo ambalo
wananchi mnatakiwa kuwa makini na kutopiga kura za hasira.
“Tunapokuja kwenu na wagombea hawa kuwanadi jambo la
busara ni kuwauliza maswali nini watafanya mkiisha wachagua kuwatumikia katika
majukumu yao kwenye mitaa yenu, lakini pia watatekeleza sera na ilani za vyama
vyao katika kuwaleta maendeleo pamoja kuwahojijinsi gani wamejipanga kuzitafutia
ufumbuzi wa haraka kero mbalimbali zilizopo kwa jamii,”alisisitiza.
Hewa aliwahasa wananchi kutopiga kura kwa ushabiki wa
kisiasa pia kwa hasira baada ya kuchochewa na baadhi ya wanasiasa badala yake
wajitokeze kuwasikiliza kwa makini wagombea wakati huu wa kampeni za kujinadi ndipo
mfanye uamuzi sahihi siku ya Desemba 14 mwaka huu ya upigaji kura ili kuwapata
viongozi bora watakaowatumikia kwa weredi.
“Pamoja na CCM kupoteza uwakilishi wa Ubunge wa
Jimbo la Nyamagana na Udiwani Kata ya Mahina tumeendelea kutekeleza ahadi zetu
kwa wananchi, lakini mimi kama Mbunge wa vitimaalum Mkoa wa Mwanza kupitia CCM
nimehakikisha utekelezaji wa daraja la Mahina unakamilika ikiwemo kumaliza
migogoro ya viwanja katika baadhi ya maeneo ya mitaa ya katani hapa,”alisisitiza.
Naye Rajabu Jumanne anayegombea nafasi ya mwenyekiti
wa mtaa wa Ipuli kwa niaba ya wagombea ujumbe wa kamati ya mtaa, akijinadi kwa
wananchi alisema kwamba amekuwa mstari wa mbere kushughulikia mgogoro wa
viwanja katika maeneo yote ya Ipuli, ambapo hadi sasa malalamiko yameisha na
wananchi wamepata haki yao.
Jumanne alisema, wananchi wa mtaa wa Ipuli na mtaa
wa jirani wa Mahina wamekuwa wakikabiliwa na changamoto mbalimbali hivyo
nivyema wakawachagua viongozi watakaoshirikiana nao kuhakikisha wanazitafutia
ufumbuzi na wananchi wanapata huduma badala ya kuchagua watu ambao wamekuwa
wakiwatelekeza wananchi na kuanza visingizio.
“Wananchi tunaomba kura zenu kwa wagombea wote wa
mitaa ya Kata ya Mahina kupitia CCM kwani tumekuwa tukishirikiana kwa karibu na
wananchi katika matatizo mbalimbali ya kijamii, tumeendelea kuwa wasikivu kwenu
na kero zote zilizojitokeza tumezishughulikia kwa kushirikiana na viongozi wa
CCM Kata na Wilaya ya Nyamagana,”alisema.
Mkutano huo wa kuwanadi wagombea wa Kata hiyo kutoka
mitaa 20 ya Kisiwani, Shigunga, Mandu, Kasota, Maswa Mashariki, Maswa Magharibi,
Sokoni, Nyanguruguru, Mahina Kati, Mahango B, Mahango C, Mahango A, Mahango,
Temeke, Susuni, Mwananchi, Igelegele, Bugarika, Ipuli na Mahina.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.