ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Friday, December 12, 2014

MWANZA KUFIKIA MALENGO YA MILENIA KUKABILIANA NA AFYA YA MAMA NA MTOTO IFIKAPO DISEMBA 2015

Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana Baraka Konisaga akifungua Mkutano huo.
Mratibu wa Afya ya mama na Mtoto mkoani Mwanza Secilia Mrema akitoa ufafanuzi mbele ya waandishi wa habari.
Kaimu Mganga Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Drt. James Kengia akitoa ufafanuzi wa maswali ya wadau waliokutana.
Bw. Stanley Matowo, mataalam wa maji kutoka sekretarieti ya mkoa wa mwanza akichangia katika kikao hicho.
Shekhe wa Mkoa wa Mwanza Hassan Fereji akiwa na Mkuu wa Wilaya ya Kwimba Seleman Mzee wakifatilia kwa karibu mtoa mada katika kikao hicho
Na: Atley Kuni-(Afisa habari Mwanza).
MKOA wa Mwanza umejiwekea malengo makubwa ili kukabiliana na afya ya uzazi na malezi bora kwa mtoto ili kuweza kufikia malengo ya milennia ifikiapo Desemba 2015.

Hayo yamesemwa na bibi Secilia Mrema wakati akiwasilisha mada kwenye kikao cha pamoja kilichokutana katika ofisi ya mkuu wa mkoa na wadau wa masuala ya afya mkoani hapa kwa ajili yakupitia mipango waliojiwekea lakini pia kupeana majukumu ili kuweza kufikia azma yao hiyo.

Mrema amesena, kutokana na hali ya uzazi salama kuwa chini ukilinganisha na mikoa jirani kama vile Kagera ndio maana wameamua kukaa pamoja ili waone kwa namna gani wanaweza kutoka mahali walipo na kufikia malengo waliojiwekea ifikiapo  mwishoni mwa 2015.

Amesema kutokana na Uelewa mdogo juu ya njia za uzazi salama kwa watoa huduma na kwa jamii, Mila na desturi zinazofanya utumiaji mdogo  wa huduma za afya ya uzazi na uzazi wa mpango, ushiriki mdogo wanaume ni  baadhi sababu kubwa iliyo wasukuma kuja na mikakati hiyo, lakini pia kutokana na mpango wa Tekeleza sasa kwa matokeo makubwa (BRN) ni njia moja wapo ya visababishi vilivyo wafanya kuja na mikakati hiyo “ Tunajua suala la afya ya uzazi ni jukumu la jamii nzima ndio maana tumeona ni vema tuka kaa wadau wote tunao husika ili tuweze kuangalia kiunaga ubaga mikakati hii tuliojiwekea.

Kutokana na changamoto hizi mkoa kwa kupitia halmashauri za wilaya umejiwekea malengo yafuatayo:-
Kupiga vita mila na desturi zinazofanya utumiaji mdogo  wa huduma za afya ya  uzazi kama  vile, uzazi wa mpango, ushirikishwaji wa wanaume, Kuongeza kiwango cha wajawazito kujifungulia kwenye vituo vya kutolea huduma za afya  kutoka 68%-80% ifikapo desemba 2015, kuongeza  kiwango cha huduma baada ya kujifungua ndani ya siku 7 kutoka 21% mpaka 62% ifikapo  Decemba  2015, kuongeza kiwango cha watoto wanaozaliwa na kina mama wenye maambukizi ya VVU kutumia  ARV (prophylaxis) kutoka 45% to 65% ifikapo Decemba 2015 kuongeza namba ya vituo vinavyotoaa huduma ya IMCI kutoka 69%-80% ifikapo Desemba 2015, mbali ya mikakati hiyo vilevile mkoa umedhamiria Kuboresha utoaji wa taarifa kwa wakati kutoka 66%-100% ifikapo Decemba 2015. 

Mrema amekwenda mbali zaidi nakusema ili waweze kufikia malengo waliojiwekea watatoa mafunzo kwa watoa huduma kuhusu (njia za kisasa za uzazi wa mpango, huduma za dharura wakati wa uchungu na kujifungua, huduma ya kumsaidia mtoto mchanga kupumua baada ya kuzaliwa, IMCI, mtuha). Aidha kupitia vyombo vya habari watatumia mwanya wakutoa elimu kwa umma ili wajue umuhimu wa afya ya uzazi lakini pia kufanya mikutano mingi ya uraghabishaji kwa umma ili ufahamu umuhimu wa masuala ya afya ya uzazi kwa mama na mtoto.

Mkoa wa Mwanza ni mojawapo ya  mikoa 6 inayo unda kanda ya Ziwa ambao una wilaya ziapatazo saba  zenye visiwa 68. Huku mkoa huo kwa mujibu wa sensa ya watu na  makaazi ya mwaka 2012 ikiwa jumla ya watu wapatao 2,772,509, idadi ya watoto chini ya mwaka mmoja ikiwa ni 104,507, na watoto  watoto chini ya miaka 5 ikiwa ni 516,998 huku  wanawake wenye umri wa kuzaa kwa maana ya umri kati ya miaka (14-49yrs)  ni 677,100. 

Mrema amesema, wastani wa watoto katika familia ni 5.4 (Fertility rate), na ukuaji wa wakazi kwa maana ongezeko la watu kimkoa ikiwa ni 3.2% kwa mujibu wa sense ya 2012, aidha mkoa pia  una jumla ya vituo vya kutolea huduma za afya 360 kati ya hivyo vituo 263 (73) % vinatoa huduma za afya ya uzazi na mtoto. 

Awali akifungua kikao hicho Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Magesa Mulongo katika hotuba yake iliyosomwa na Mkuu wa Wilya ya Nyamagana alisema ni jukumu la kila mmoja wetu “kujihoji ni kwa vipi mama apoteze maisha ili hali kila mmoja wetu anajua kuwa mama ndiye anaye tengeneza maisha”? aidha  amesema kuwa kutokana na lengo la nne la millennia kugusa suala nyeti kama hili ndio maana kama taifa tayari tathimini ilifanyika ambapo Wakuu wa Mikoa yote Tanzania Bara, Makatibu Tawala na Waganga Wakuu wa Mikoa Tanzania walikutana na Mheshimiwa Rais tarehe 15 Mei, 2014 na kupewa taarifa ya tathimini hiyo na kujadili mkakati mpya ulioboreshwa wa kitaifa katika kufikia lengo la 4 na la 5. 

Ifikapo mwishoni mwa mwaka 2015, “Pamoja na mengine tuliyokubaliana mbele ya Mheshimiwa Rais, suala la uwajibikaji lilipewa kipaumbele ambapo kila mmoja wetu aliweza  kupata uzoefu wa mikoa mingine, mfano Singida na Mara jinsi walivyofaulu katika suala la afya ya uzazi.

Kikao hicho cha siku moja kimewakutanisha Viongozi wa dini, wakuu wa Wilaya, Wakurugenzi wa halmashauri, wenyeviti wa halmashauri, waganga wakuu wa wilaya na waratibu wa afya ya uzazi wa wilaya pamoja na wataalam kutoka sekretarieti ya mkoa wa Mwanza.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.