ZOEZI LA UCHUNGUZI WA AFYA YA MACHO NA UPASUAJI WA MACHO KWA WATOTO MIKOA YA KANDA YA ZIWA NA MAGHARIBI UMEENDELEA TENA LEO KATIKA HOSPITALI YA SEKOU TOURE JIJINI MWANZA.
HOSPITALI YA MKOA WA MWANZA SEKOU TOURE.
UPASUAJI HUO UNAOFADHILIWA NA KAMPUNI YA MTANDAO WA SIMU NCHINI TIGO UMEFANYIKA KWA AWAMU YA PILI LEO UKIWASHIRIKISHA MADAKTARI BINGWA KUTOKA CCBRT KWA KUSHIRIKIANA NA MADAKTARI WA HOSPITALI YA SEKOU TOURE MKOA WA MWANZA, UMEONEKANA KUHITAJI MUDA ZAIDI KWANI IDADI KUBWA YA WATOTO WAKIWA NA WAZAZI WAO WAMEONEKANA KUENDELEA KUMIMINIKA HOSPITALINI HAPO TENA WENGINE KUTOKA MBALI WAKIWA NA MATATIZO YA MTOTO WA JICHO NA MAGONJWA MENGINE YA MACHO.
AIDHA MPANGO HUO ULIOANZA JANA TAREHE 8 NA KUPANGWA KUHITIMISHWA LEO TAREHE 9 NOV 2010 UKIWAHUSISHA WATOTO WA CHINI YA MIAKA 16 UMEONEKANA KUWAVUTA PIA WATU WENYE UMRI ZAIDI YA UMRI ULIOTAJWA HALI INAYOPELEKEA KUWAPA CHANGAMOTO WAHUSIKA WA MPANGO HUO KUFIKIRIA TENA ZAIDI JUU YA MATIBABU AWAMU NYINGINE KWA WAKAZI WA KANDA YA ZIWA NA MIKOA YA MAGHARIBI.
WANANCHI WAKIWA WAMEJIPUMZISHA KUSUBIRI HUDUMA.
TIGO IMEAMUA KUSHIRIKIANA NA TAASISI YA CCBRT ILI KUONGEZA UGUNDUZI WA TATIZO LA MTOTO WA JICHO KWA WATOTO NA PIA KUFADHILI MAFUNZO YA WIKI MBILI YA KOZI YA HUDUMA ZA UZAZI KWA WAKUNGA 10, IKIWEMO PIA NA UFADHILI WAO WA KLINIKI ZA MACHO AMBAZO HUTOA HUDUMA ZA UCHUNGUZI NA TIBA YA MATATIZO YA MACHO KWA WATOTO HASA TATIZO LA MTOTO WA JICHO.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.