Katibu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. Thomas Kashililah akizungumza na waandishi wa habari kuhusu mpangilio mzima wa shughuli za bunge katika mkutano wa kwanza wa Bunge Utakaoanza Tarehe 8-17 Novemba 2010 mjini Dodoma.kushoto ni Mkuu wa Kitengo cha sheria anaitwa Oscar Mtenda.
Dk Dr. Thomas Kashililah amesema kwamba leo tarehe 8-11-2010 amepoka barua rasmi kutoka wa Rais wa Jamhuri ya Muuungano wa Tanzania Jakaya Kikwete akilitisha kikao cha bunge la jamhuri la Muungano wa Tanzania ambapo wabunge wataanza kuelekea Mkoani Ddodoma tayari kabisa kuanza kikao kipya cha bunge kwanzia Tarehe 9-11-2010 na kazi ya kuanza kusajili wabunge wateule itaanza rasmi mpaka tarehe 10-11-2010
Na siku ya alhamisi kutafanyika mikutano ya kamati za vyama vya siasa kupokea majina ya wagombea uspika wa bunge la jamhuri la muungano wa Tanzania na siku ya ijumaa tareeh Tarehe 12-11-2010 utaanza mkutano wa kwanza wa bunge la jamhuri la muungano wa Tanzania na kusomwa Tangazo la Rais Jakaya kikwete kuliita bunge na kufanya uchaguzi wa Spika na baada ya kuchaguliwa spika atakula kiapo ambapo wabunge nao wataanza kuapishwa rasmi Jumamosi Tarehe 13-11-2010 na 15-11-2010 hadi jumanne ya 16-11--2010 asubuhi kikifatiwa na tukio la kuthibitishwa kwa jina la Waziri Mkuu na Waziri Mkuu huyo kutoa Neno la Shukrani na Kumalizia na Uchaguzi wa Naibu Spika.
Tarehe 17-11-2010 Waziri Mkuu ataapishwa katika ikulu ya chamwino saa nne na saa kumi jioni ni tukio la Rais Jakaya Kikwete kulihutubia Bunge katika Ukumbi wa Bunge na Baada ya Rais Jakaya Kikwete kumaliza kulihutubia Bunge Waziri Mkuu atatoa Neno la Shukrani na kutoa hoja na kuahirisha Bunge.
Habari/Picha na Benjamin Sawe-MAELEZO.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.