"Mafanikio ya mapinduzi haya yanategemea mshikamano wa walengwa, tunatumaini yatachangia kwa ujumla wamapinduzi haya na kuwafungulia jia ya kushiriki, wale watakaohamasika"
"Sababisha Mapinduzi ya Uchumi na POSO" ni kampeni ya kitaifa ya kufikisha kwa wananchi fursa za uwekezaji na uwezeshaji silisowekwa na sera hii kwa wananchi ili wazitumie kujitajirisha kiadilifu.
Kampeni hii inakusudia kujenga uelewa wa Watanzania walio wengi ili kushiriki kikamilifu katika ujenzi, umiliki, usimamizi na uendelezaji wa mitaji, vitegauchumi, soko, biashara na ajira.
Kupitia Kampeni hii kila Mtanzania atawezeshwa kuwa Mtajirishaji anayefanikisha ujenzi wa Nguvukazi Bora inayowajibika kutoa huduma, kuzalisha na kusambaza bidhaa bora zinazohimili ushindani katika soko la ndani na nje ya nchi.
Kwa kifupi, Mtajirishaji ni mtu mwadilifu, mwenye werevu wa kiwangocha juu cha kutumia mazingira yanayomzunguka na ya utandawazi kufungamana katika ubia unaofanikisha uwekezaji unaoibua na kuendeleza Ubunifu, uvumbuzi na Ujuzi (UUU)unaobadili Wazo, taaluma na Rasilimali kuwa Huduma, Bidhaa na Mali Bora zinazouzika kwa Faida inayotengeneza Hazina ya kutajirisha vizazi vyote.
Kampeni hii ni sehemu ya utekelezaji wa mpango wa ujenzi wa ajira zinazowezesha wananchikufungamana na kujitajirisha kiadilifu, chini ya MILIKI mfumo wa UTAJIRISHAJI, unaoinua uwezo wa Watanzania, wa kubuni, kuanzisha, kuendeleza na kusimamia vitegauchumi nabiashara, kujenga na kumiliki mitaji ya uwekezaji, pamoja na kuhimili ushindani wa soko kwa kutumia rasilimali chache kati ya nyingi zinazotuzunguka.
Wabia wakuu katika utekelezaji wa mpango huu nikampunizilizoanzishwa na wananchi chini ya ushirikiano wa GODTEC (T) CO. LTD na Serikali kupitia Wizara ya Habari, Vijana, utamaduni na Michezo.
Meza ya wadau wa SUSO. |
Wanahabari washiriki wa mkutano. |
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.