TAARIFA KWA VYOMBO VYA
HABARI
Toleo la Leo
SAFARI
LAGER YATANGAZA RASMI UPATIKANAJI WA FOMU ZA PROGAMU YA SAFARI LAGER WEZESHWA
MSIMU IV.
Dar es Salaam, Jumanne Januari 6, 2015: Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) kupitia bia yake ya
Safari Lager leo imetangaza rasmi upatikanaji wa fomu za programu yake ya
Safari Lager Wezeshwa kwa msimu wa nne
kwa wajasiriamali wadogo wadogo na wa
kati Nchini.
Akizungumza na waandishi wa habari, Meneja
wa bia ya Safari Lager Bi. Edith Bebwa
alifafanuwa ya kwamba “ Fomu za ushiriki zitapatikana kwenye mabohari ya
TBL, Mawakali wa kusambaza bia, kwenye mtandao wa www.wezeshwa.co.tz . Fomu hizo
zichukuliwe, zijazwe na kurejeshwa kwenye vituo vilivyotajwa hapo juu au kwa
njia ya posta kwa sanduku la posta (Safari Lager Wezeshwa msimu wa nne,Tbl Dar
es Salaam,P.o Box 9393 DSM).
Alisema Bi Edith, hii ni hazina tosha kwa wajasiriamali wadogowadogo nchini
kwani itarahisisha kazi kwa kuwepo na
vitendea kazi bila ya kutumia nguvu nyingi”.
Programu hii ni msimu wa nne tangu
kuanzishwa kwake na imeleta mafanikio
makubwa kwa wajasiriamali waliopata uthubutu wa kujaribu kujiunga na hatimae
kuongeza uchumi wa nchi.
Programu hii itafanyika takribani mikoa yote ambapo itawapa fursa
wajasiriamali wa aina zote bila kujali fani,kabila wala jinsia kujaza fomu kwa usahihi na kamilifu kisha kuzirudisha mahala husika na baadae
waliokidhi nafasi zinazohitajika kuchaguliwa kisha kupewa mafunzo mafupi pamoja na kukabidhiwa ruzuku zao alisema Bi Edith.
Meneja wa bia ya Safari Lager, Edith Bebwa alimaliza kwa kutaja tarehe ya
mwisho wa kurejesha fomu kuwa ni 20,Februari 2015 hivyo wajasiliamali
wanapochukua fomu wakumbuke pia muda wa kuzirejesha walipozitoa.
Nae kiongozi wa wataalamu wa ushauri wa biashara kutoka kampuni ya TAPBDS,
Bwana Joseph Migunda alisema kuwa “Zoezi hili linahusisha wataalamu wenye uwezo
na uzoefu mkubwa katika kushauri na kusaidia ukuzaji wa sekta ya biashara ndogo
na kubwa. Hivyo aliomba wajasiriamali wote kuitumia fursa hii kushiriki kwa
kuzingatia vigezo vilivyoainishwa kwenye fomu ya ushiriki. Wenye nia ya kufika
mbali kibiashara na wenye malengo ya
kuisaidia jamii inayowazunguka wasisite kuchangamkia fursa hii”.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.