ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Friday, April 6, 2018

VIDEO: MASHABIKI MWANZA WALIA NA MBAO FC.


JINAMIZI la kutoka sare  limezidi kuiandama Timu ya Mbao Fc ya jijini Mwanza baada ya kutoka sare na timu ya Lipuli kutoka mkoani Iringa katika mtanange wa Ligi kuu Soka Tamzania Bara uliopigwa Uwanja wa CCM Kifrumba jijini hapa.

Katika vipindi vyote vya mchezo timu zote zilionekana kuwa na safu butu hasa Mbao Fc iliyoonekana kuingia mara kadhaa langoni mwa timu ya Lipuli lakini uwezo wa washambuliaji wake kufumania nyavu ulikuwa mdogo.

Lipuli walionekana kucheza kwa tahadhri `ili wasifungwe wakiwa ugenini huku wakicheza kwa kujihami zaidi kuliko kushambulia wakihakikisha washambuliaji wa Mbao wasipenye na kuleta madhara.

Hadi mwisho wa mchezo Mbao FC imelazimishwa sare ya 0-0 na Lipuli FC ya Iringa.

Kwa sare hiyo, Mbao FC inabaki kwenye eneo la hatari ya kushuka daraja, ikifikisha pointi 20 baada ya kucheza mechi 23 na kuendelea kukamata nafasi ya 14 katika ligi hiyo yenye timu 16, mbele ya Njombe Mji FC yenye pointi 18 za mechi 22 na Maji Maji FC pointi 16 za mechi 22.


Lipuli FC yenyewe inayofundishwa na wachezaji wake wa zamani wa Simba SC, Suleiman Matola na Amri Said imefikisha pointi 28 baada ya kucheza mechi 23 na kuendelea kukamata nafasi ya saba, ikiwa juu ya Mbeya City na Ruvu Shooting ya Pwani zenye pointi 25 kila moja baada ya kucheza mechi 22 pia. 

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.