Mwenyekiti wa Bodi ya Chama Kikuu cha ushirika cha Kagera (KCU) Ndg Onesmo Niyegila (Kulia) akizungumza na waandishi wa habari wakati akitoa ufafanuzi kuhusu malipo ya awali ya kahawa ya wakulima wa Chama Kikuu cha Kagera KCU (1990) Ltd, Leo 7 Aprili 2018, Mwingine ni Kaimu meneja Mkuu wa Chama Kikuu cha ushirika cha Kagera (KCU) Ndg John kanjagaile. Picha Zote Na Mathias Canal, WK
Waandishi wa habari wakifatilia Mkutano wa Mwenyekiti wa Bodi ya Chama Kikuu cha ushirika cha Kagera (KCU) Ndg Onesmo Niyegila wakati akitoa ufafanuzi kuhusu malipo ya awali ya kahawa ya wakulima wa Chama Kikuu cha Kagera KCU (1990) Ltd, Leo 7 Aprili 2018, Katika Ukumbi wa Ofisi za Wizara ya Kilimo (Kilimo 4).
Na
Mathias Canal, WK-Dodoma
Mwenyekiti wa Bodi ya Chama
Kikuu cha ushirika cha Kagera (KCU) Ndg Onesmo Niyegila ametoa ufafanuzi kuhusu
malipo ya awali ya kahawa ya wakulima wa Chama Kikuu cha Kagera KCU (1990) Ltd
kama ilivyojadiliwa kwenye Mkutano wao Mkuu tarehe 27/03/2018.
Amebainisha hayo wakati
akizingumza kwenye mkutano na waandishi wa habari Mjini Dodoma na kusema kuwa Chama
Kikuu cha Ushirika cha Kagera si Kampuni ya kununua kahawa bali ni ushirika wa
wakulima wadogo wadogo wenye lengo la kuunganisha nguvu zao kwa pamoja katika kuhudumia zao la kahawa na kuliwasilisha sokoni kwa utaratibu
wenye tija endelevu na kisha kugawana mapato baada ya kufanya mauzo.
Alisema bei halisi ya mkulima
kwa upande wa Ushirika inapatikana mara baada ya mauzo ya kahawa kufanyika ambapo wakulima hulipwa malipo ya mwisho kwa kadri
ya bei ya kuuzia iliyopatikana sokoni na hesabu ya mwisho kuwasilishwa kwenye
mkutano mkuu.
Hivyo kwa vile mchakato
wa mauzo huchukua si chini ya kipindi cha mwezi mmoja tangu mkulima awasilishe
kahawa yake kwenye ushirika hadi malipo ya mwisho kufanyika, basi ili
kumuondolea mkulima adha ya kusubiri malipo yake yote baada ya mauzo wakati
anahitaji kujikimu na kukidhi mahitaji yake muhimu, wakulima wenyewe kwa utashi
wao kupitia Mkutano Mkuu, wanajadili
malipo ya awali atakayotanguliziwa mkulima wakati anasubiri malipo ya mwisho.
Niyegila alibainisha
kuwa mnamo tarehe 27/03/2018, Chama Kikuu cha Kagera kilifanya Mkutano wake
Mkuu ambao pamoja na mambo mengine wanachama walijadili malipo ya awali ya
mkulima (Advance Payments). Katika makisio hayo, Menejimenti na Bodi ya KCU (1990) Ltd
walipendekeza malipo ya awali yawe ni TZS 1,000 kwa kilo moja ya kahawa ya
maganda.
Alisema kuwa baada ya
mjadala, wanachama waliagiza kupitiwa upya kwa makisio hasa katika upande wa
malipo ya awali na kuangalia namna ya kupandisha kiwango cha malipo ya awali. Aliongeza
kuwa Kiwango kipya pendekezwa kitawasilishwa kwa Mrajis wa Vyama vya Ushirika
nchini kwa ajili ya kuidhinishwa.
Alisisitiza kuwa kile
kilichojadiliwa kwenye Mkutano Mkuu wa wanachama si tangazo la bei bali ni
malipo ya awali kwa mkulima ambapo Kwa mujibu wa sheria, bei elekezi ya zao la
kahawa inatolewa na Bodi ya Kahawa Tanzania kwa utaratibu wa ushirika, bei
halisi itajulikana mara baada ya mauzo ya kahawa kufanyika sokoni na si
vinginevyo.
Niyegila aliongeza kuwa
kwa utaratibu wa sasa wa Serikali, kahawa yote itakusanywa kupitia kwenye Vyama
vya Ushirika na kupelekwa sokoni Manispaa ya Moshi Mkoani Kilimanjaro ambapo
wanunuzi wote watanunulia hapo mnadani.
Kwa mantiki hiyo,
hakuna mkulima yeyote atakayeruhusiwa kuuza kahawa nje ya mfumo wa ushirika
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.