WAKAZI WA MTAA WA IBISABAGENI KATA YA IBISABAGENI
KATIKA HALMASHAURI YA WILAYA YA SENGEREMA WAMEAMUA KUJITOLEA KULIMA NA KUFUNGUA
BARABARA IKIWA NI KATIKA JUHUDI ZA KUJILETEA MAENDELEA NA KUONDOA KERO ZA
MAWASILIANO KATIKA MTAA HUO
Akizungumza wakati wa zoezi hilo leo lililofanyika mapema
asubuhi mwenyekiti wa mtaa wa IBISA BAGENI
MH STANNRY KAKERE amesema kuwa kupitia mikutano mbali mbali wameadhimia
kulima barabara ili kujiletea maendeleo katika
mtaa wao.
Pamoja na hayo mwenyekiti huyo wamewashauri baadi ya
viongozi kusimamia maendeleo katika maeneo yao hasa katika swala la ulinzi na
usalama na wananchi na atakayeshindwa
hatua za kisheria zichukuliwe dhidi yake.
Kwa upane wawao wananchi wa kata hiyo wao wamesema kufunguliwa
kwa barabara hizo kutachochea maendeleo
yao na kusaidia kuondoa kero ya
kuzunguka umbali mrefu kwenda hospitali teule ya MISSION iliyopo karibu kata
jirani ya MISSION.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.