ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Friday, April 6, 2018

MGUNDUZI WA TANZANITE AANGUKIWA NA NEEMA YA MAGUFULI.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli ameahidi kumpatia pesa kiasi cha Tsh. Milioni 100, Mgunduzi wa Madini ya Tanzanite, mzee Jumanne Ngoma imsaidie katika matibabu ya ugonjwa wake unaomsumbua wa kupooza.

magufuli amesema hayo leo, Aprili 6, 2018 katika eneo la Simanjiro ambako anazindua Ukuta uliojengwa kuzungushiwa Migodi ya Tanzanite, Mirerani ili kuzuia utoroshwaji wa madini hayo.


“Madini haya yalivumbuliwa na mzee Jumanne Ngoma mwaka 1967, na kupeleka sampuli kwa Geologist (mtaalam wa miamba) kwenda kuyapima, pamoja na kutambuliwa na Baba wa Taifa, Mwl Julius Kambarage Nyerere kwenye barua aliyoisani Oktoba 8, 1980 akitambua kazi nzuri ya mzee Ngoma.

“Hata alipoyavumbua hakujua yatakuwa na thamani kubwa kiasi hicho, lakini mzee Ngoma hakufaidika chochote, sasa naambiwa amepooza, nitampatia shilingi milioni 100 zikamsaidie katika matibabu,” alisema Magufuli.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.