
Imetajwa kuwa kukosekana kwa uaminifu, matumizi mabaya ya madaraka sambamba na migogoro isiyoisha ndani ya vilabu na vyama vya michezo mkoani Mwanza ndiyo chanzo kikuu cha kuporomoka kwa michezo hususani soka kwa jiji la Mwanza.
Hayo yamebainishwa leo na mkuu wa mkoa wa Mwanza Injinia Ernest Ndikilo wakati akifungua Mkutano Mkuu wa Chama cha soka mkoa wa Mwanza (MZFA) unao kaa kila mwaka kuweka mikakati ya maendeleo na kujadili mstakabali mzima wa maendeleo ya soka.






Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.