ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Friday, November 25, 2022

"KILA UHAI UNA THAMANI TOKOMEZA UKATILI DHIDI YA WANAWAKE NA WATOTO" SIKU 16 ZA KUPINGA UKATILI.

Tumekusanyika hapa leo tukiungana na mataifa mengine kote duniani kuadhimisha Kampeni ya Siku 16 za Uanaharakati Dhidi ya Ukatili wa Kijinsia ambapo kitaifa unaizindua wewe mwenyewe leo hapa katika viwanja vya Klabu ya Viongozi (Leaders Club) . 

Leo ni siku ya Kimataifa ya Kupinga Ukatili Dhidi ya Wanawake ambayo ndio siku ya kwanza katika kuadhimisha kampeni ya siku 16 za Uanaharakati. Anna Kulaya(Mratibu wa WiLDAF) 

Ingawa tunafuraha kuona umati mkubwa huu na wewe mwenyewe mgeni rasmi ukijumuika nasi kwenye uzinduzi huu, mioyoni tumejaa machungu tele. Ni hali yakusikitisha kuwa karne hii ya 21 ya ulimwengu uliostaarabika, bado kuna matukioya ukatili wa kijinsia kwani tunaamini yanazuilika

Kauli mbiu ya kampeni ya mwaka huu ni “Kila Uhai Una Thamani! Tokomeza Ukatili Dhidi ya Wanawake na Watoto.” Anna Kulaya (Mratibu wa WiLDAF) #PingaUkatiliOkoaMaisha #16DaysOfActivism 

Kauli mbiu hii imelenga kuhamasisha kila mtu, jamii, taasisi na serikali kuwa sehemu ya kuwajibika kutokomeza vitendo vyote vya ukatili kwani madharayake ni makubwa na mwisho hupelekea vifo hasa kwa wanawake nawasichana

Miaka ya hivi karibuni kumekuwa na vitendo vya ukatili wa kijinsia,Mathalani ripoti ya mwaka 2021 jeshi la polisi lilionyesha jumla ya watu 29,737 walifanyiwa ukatili wa kijinsia kati yao 20,897 ni wanawake, 8,476 wanaume. 

Ambapo kati yao mauaji ya vikongwe ni 118. Asilimia 68.6 ya mauaji yaliyoripotiwa yalikuwa ni dhidi ya wanawake. Mwaka 2020, mauaji yaliyotokana na migogoro ya majumbani na wivu wa mapenzi ni asilimia 26% ya mauaji yote yaliyoripotiwa katika Jeshi la Polisi. 

Naye Waziri wa Wizara ya Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wanawake na Makundi Maalumu Dkt Dorothy Gwajima Ameiongeza WiLDAF na Mkuki kwa uratibu na kufanikisha uzinduzi wa siku 16 za unaharakati vile vile amepongeza wazo la msafara wa kupinga ukatili wa kijinsia vilevile amesema atashiriki kwenye baadhi ya mikoa.

Wana MKUKI  tumejipanga kutumia kampeni hii kufanya shughuli mbalimbali ikiwemo Msafara wa kampeni wa kupinga ukatili wa kijinsia ambao utapita mikoa (Pwani,Morogoro,Dodoma,Shinyanga,Geita,Mara na Arusha) 

Msafara huu utatembelea jamiii, mashuleni, kwenye vituo vya mabasi na maeneo ambayo yanaonesha Kombe la Dunia na kwa kutumia njia hii tutaweza kufikia wanaume wengi zaidi na kuhamasisha mabadiliko ya kifikira, kimtazamo namatumizi mabaya ya mamlaka/power walizonazo katika kulinda wanawake nawatoto. 

Tarehe 8 Desemba tunategemea kuwa na tuzo maalum kwa vinara wanaolinda wanawake, watoto na kuzuia ukatili wa jinsia.Tuzo hii imeanzishwa na wana MKUKI kwa kushirikiana na wadau wa maendeleowakiwemo UNFPA na LSF ikiwa ni sehemu ya kutambua mchango wa watukatika jamii zetu wanaofanya kazi kubwa ya kuzuia na kutokomeza vitendo vyaukatili wa kijinsia. Anna Kulaya(Mratibu wa WiLDAF)#PingaUkatiliOkoaMaisha 

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.