ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Thursday, November 24, 2022

RAIS WA BRAZIL AKIMBILIA KORTINI KUPINGA MATOKEO YA UCHAGUZI AKITAKA UFUTWE

 


Rais wa Brazil anayeondoka Jair Bolsonaro amewasilisha ombi katika mamlaka ya uchaguzi ya Brazil kupinga rasmi matokeo ya kura ya urais ya Uchaguzi Mkuu wa 2022. Rais wa Brazil anayeondoka Jair Bolsonaro ataka matokeo ya urais yafutwe.

Bolsonaro alipoteza kura ya marudio kwa ushinde mwembamba mnamo Oktoba 2022, kwa mpinzani wake Luiz Inacio Lula da Silva, almaarufu "Lula," ambaye anatazamiwa kuapishwa rasmi kuwa rais mnamo Januari 1. 

Kufuatia ushinde huo, Bolsonaro alionekana kukiri wazi kuwa anakubali kushindwa akisema ataendelea kutimiza amri zote za katiba. Kauli yake iliwafanya waangalizi kuamini kuwa atamwachia Lula madaraka kwa amani. 

Hata hivyo, mnamo Jumanne, Novemba 22, Bolsonaro na kiongozi wa chama chake cha mrengo wa Liberal waliwasilisha malalamishi wakidai kuwa baadhi ya mashine za kupigia kura zilikumbwa na hitilifu na kura zote zilizopigwa kupitia mashine hizo zinapaswa kubatilishwa. 

Akirejelea ripoti ya ukaguzi uliofanywa na kampuni iliyoajiriwa na chama cha Bolsonaro, walalamishi wanadai kuwa iwapo kura hizo zitafutwa, basi Bolsonaro angeibuka mshindi.

 Wakijibu ombi la Bolsonaro, maafisa wa tume ya uchaguzi walisema kwa kuwa mashine hizo ndizo zilizotumika katika duru ya kwanza ya uchaguzi, Bolsonaro na chama chake lazima warekebishe malalamiko yao ili kujumuisha matokeo hayo kupitia mahakama. 

Mahakama ya Upeo ya Uchaguzi ya Brazil, imempa Bolsonaro na walalamishi wenzake saa 24 kurekebisha maombi yao. Uchaguzi mkuu wa Oktoba ulikumbwa na ushindani mkali na ulikujia wakati kulikuwa na hali ya wasiwasi na mgawanyiko wa kisiasa nchini humo, ambayo imekuwa ikikabiliwa na mfumuko wa bei, na kuongezeka kwa umaskini. 

 Lula da Silva alipata zaidi ya kura milioni 60 kulingana na matokeo ya mwisho ya halmashauri ya kusimamia uchaguzi Brazil. Kura hizo zilikuwa nyingi zaidi katika historia ya Brazili na kuvunja rekodi yake mwenyewe kutoka 2006. 

Ushindi wake unakujia baada ya kufungwa jela mnamo 2018, na alikaa gerezani kwa zaidi ya miezi 18 kwa tuhuma za ufisadi. Lula alipoteza urais mara tatu na hatimaye akafanikiwa kushinda mnamo 2002 na tena miaka minne baadaye.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.