Nape Moses Nnahuye, mtoto wa Brigedia Moses Nnahuye.
Umelinda
heshima ya baba yako mwanamapinduzi, umeonyesha damu ya mjali utu, naam
kizazi cha haki, kikao cha hekima. Busara si mlima lakini pia siyo
mtelemko.
Jina lako halitafutika katika nchi takatifu Tanzania. Kama kwa baba na mwana.
Cheo ni nini?
Hofu ni nini?
Aibu ni kitu gani?
Naam umetenda kiutu, umeonysha ujemedari. Wewe ni mjenga nchi, popote ulipo, kwanafasi yoyote, kwa jina lolote.
Zile siku na zije, majemedari wamekuja na wapo tayari.
Nawaende washibao kwa dhuruma, ghiliba, choyo, ubinafsi, visasi, ukatili, tamaa mbaya, fitina, huzushi na laghai.
Kila mwenye mapenzi mema, aonaye sasa na hata halfajiri atasimama na wewe.
Asubuhi njoo, umande wa kesha utaondoka..........Lucas Haule.
Nape hongera.
Heri kufukuzwa uwaziri kuliko kukanyaga sheria na Katiba ya Tanzania,
Mungu wetu aliye juu yetu wote hatakuacha.
Kumbuka umewekwa pembeni kutokana na kusimamia heshima ya serikali.
Umetunguliwa uwaziri kutokana na kupigania haki, utu na heshima ya Watanzania.
Kazi yako imekujengea heshima ya pekee mbele ya wanahabari na Watanzania
Umekuwa Waziri wa Habari, Utamaduni na Michezo wa kupigiwa mfano katika zama hizi.
Ananilea Nkya
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.