ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Saturday, March 25, 2017

H BABA ASHUHUDIA JEMBE MEDIA GROUP IKIICHANACHANA SAHARA MEDIA GROUP 5-2 NDANI YA DIMBA JIPYA LA NYAMAGANA.



Wachezaji wa Jembe Media Group wakimwagia maji mfungaji wa goli la nne na la tano Mbaba Vc mara baada ya ushindi wa kishindo goli 5-2 dhidi ya Sahara Media Group mchezo uliochezwa dimba la Nyamagana jijini Mwanza.

Michezo siku zote imekuwa sehemu ya kuunganisha watu mbali mbali hasa wale watu ambao wanaonekana kuwa na ushindani wa kikazi, kibiashara au kazi nyingine,Michezo imekuwa ikitumika kuwa chanzo cha kusogeza ukaribu baina ya vyombo hivi.
Kikosi Cha Jembe Media Group.
Kikosi cha Sahara Media Group.
 Katika zama hizi kutoka Jijini la miamba .....Mwanza ni wazi kila mtu anafahamu mapinduzi makubwa katika tasnia ya Habari ambayo yamekuja baada ya radio Jembe Fm chini ya Mkuu wake Dr. Sebastian Ndege kutia maguu katika uwekezaji eneo hilo, Pia ni wazi kila mtu anafahamu ukongwe wa Chombo cha Habari cha Sahara Media Group ambayo inamiliki Radio Free, Kiss Fm, Star Tv na vyombo vingine chini ya mtaalamu Dkt. Anthony Diallo.





Vijana wakali wasio na maneno saaaana zaidi ya vitendo Dr. Ndege wamefanya yao.
 
Leo katika uwanja wa Nyamagana uwanja ambao umewekewa Nyasi Bandia na kukamilika hivi karibuni, leo umeweka moto ambapo Jembe Media Group ilikuwa ikicheza dhidi ya Sahara Media Group ambapo mpaka dakika Tisini za mchezo zinakamilika Jembe Media Group ikaibuka na ushindi wa Magoli (5 -2).
Juma Ayo alikuwa wa kwanza kufungua lango la magoli kwa Jembe Media Group ikiwa ni dakika ya 18 tu ya mchezo.
Kasi ya mchezo wa leo ilinogeshwa na team kapten wa Jembe Medi Group Juma Ayo ambeye alikuwa akilinyanyasa mwa-mwi lango la Sahara Media Group ya Jijini Mwanza.
Sahara Media hapa walikuwa wameweka kambi katika lango la Jembe Media kiasi cha kusababisha upatikanaji wa goli la pili wakiiacha Jembe Media waliokuwa nyuma muda huo kwa tofauti ya goli 1-2
Si kwa service hizi mchezaji lazima upone....Mshambuuliaji machachari wa Jembe Media Group Juma Ayo akipata usaidizi chini ya team ya huduma ya kwanza Jembe Family.
Kama mtu anabazidEi hivi...........
Pasha pasha ....kutoka kulia Dj Scorpion, Mbaba Vc na Chomo.


Emma The Gooner (L) na Sisco (R)
Pasha pasha......
Chini ya kocha wa Wakata Umeme.



Mfungaji wa goli la 4 na la 5 Mbaba Vc akiwa juu ya mikono ya wana-Jembe Media Group mara baada ya kuibuka washindi.

HureeeeeeEeeeee......!!

Kocha wa Sahara Media akifanya mazungumzo na wandishi wa habari mara baada ya mchezo.

Kocha mchezaji wa Jembe Media Group Albert G. Sengo akitoa tathimini ya mchezo dhidi ya Sahara Media Group, baada ya ushindi wa 5-2.

Ilikuwa ahadi hatimaye imekuwa ukweli mmoja kati ya wasanii nembo ya mkoa wa Mwanza HBaba (katikati mwenye ndevu style) amesafiri toka makazi yake ya sasa jijini Dar es salaam hadi Rock City kwaajili ya ku-show love kwa kipute hiki.
Chriss The Dj on the ball.
Mapemaaa........
Hatariiiiii..
Mpaka kieleweke.
Mshambuliaji wa Sahara Media Group akimtoka beki wa Jembe Media Ramadhani (aliyelala chini)
Halo halo.....
Benchi la timu ya Sahara Media Group likiongozwa na Kocha Abdalah Tilata.
Mchezo ni undugu kocha wa Sahara, Abdalah Tilata (L) na Kocha wa Jembe, Albert G. Sengo
Kila Kitu balaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa!!!
 

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.