Kampeni hiyo ambayo itafanywa kwa
wakati mmoja na wahudumu wa kujitolea 190,000 kwa kutembea kwa miguu,
baiskeli na njia zingine zozote, ni katika harakati za kuutokomeza
kabisa ugonjwa huo katika nchi zilizobakiwa na waathirika wa ugonjwa huo
ambao WHO inasema bado ni tishio kubwa kwa watoto walio na umri wa
chini ya miaka mitano.
Mashirika hayo yamesema mapigano katika
jimbo la Borno nchini Nigeria yalisababisha watoto wanne kupooza mwaka
2016 kutokana na ukosefu wa chanjo, eneo pekee ambalo kirusi cha Polio
bado kinatishia maisha, na iwapo hakitashughulikiwa haraka, eneo hilo na
maeneo yaliyo jirani yatakuwa hatarini kuambukizwa. Jimbo la Borno ni
ngome ya kundi la kigaidi la magaidi wakufurishaji wa Boko Haram.
Mtoto aliyepooza kutokana na polio
Mtoto aliyepooza kutokana na polio
Ili kufanikisha kampeni hiyo, mashirika
hayo yamesema ushirikiano wa serikali kuu hadi za mashinani unahitajika
ili kuweza kumfikia kila mtoto.
Nchi hizo 13 ni Benin, Cameroon, Jamhuri
ya Afrika ya Kati CAR, Chad, Côte d'Ivoire, Jamhuri ya Kidemokrasia ya
Congo DRC, Guinea, Liberia, Mali, Mauritania, Niger, Nigeria na Sierra
Leone.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.