Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), limempongeza Mheshimiwa Dk.
Harrison Mwakyembe kwa kuteuliwa kuwa Waziri wa Habari, Utamaduni,
Sanaa na Michezo.
Katika taarifa iliyotolewa leo kwa wana habari, imesema kuwa shirikisho
hilo linaamini chini ya uongozi wake mahiri Tanzania itapiga hatua kubwa
zaidi katika maendeleo ya michezo.
Naye Rais wa TFF, Jamal Malinzi kupitia mtandao wa twitter amesema "TFF
inampongenza Dkt. Harrison Mwakyembe kwa kuteuliwa kuwa Waziri wa
Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo.Tunakuombea mafanikio makubwa.Amina."
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.