Raia walioathiriwa na janga la mafuriko mashariki mwa Uganda wameilaumu serikali ya nchi hiyo kwa kuchelewa kupeleka misaada katika maeneo hayo ambapo mamia ya familia zimebaki bila makazi.
Ripoti mbalimbali kutoka nchini Uganda zinasema kuwa, waathiriwa wengi wa mafuriko hayo yaliyosababishwa na mvua zinazoendelea kunyesha wameomba hifadhi kwenye shule na makanisa.
Wakizungumza na duru za habari, baadhi ya waathiriwa mafuriko hayo wamesema kuwa, hawajapokea msaada wowote kutoka serikalini tangu Ijumaa iliyopita licha ya serikali kufahamu hali hayo na mazingira magumu wanayokabiliwa nayo.
Taarifa zaidi zinasema kuwa, baadhi ya waathiriwa wamechukuliwa na ndugu zao kwa ajili ya kuwapa hifadhi huku wengine wakibaki hawana makazi, chakua wala mavazi.
Tunaiomba serikali itufikishie misaada haraka kwani hali yetu ni mbaya mno, amesema mmoja wa waathiriwa wa mafuriko hayo alipozungumza na vyombo vya habari.
Mvua kubwa zinazoendelea kunyesha katika Ukanda wa Afrika Mashariki zimekuwa na maafa makubwa pia katika nchi jirani ya Tanzania.
Ripoti zinasema kuwa, idadi ya watu waliofariki dunia kutokana na mvua kubwa zinazoendelea kunyesha nchini Tanzania imepindukia 30 huku baadhi ya maeneo yakiharibiwa vibaya na mafuriko.
Serikali ya Tanzania imewaonya na kuwataka wananchi wanaoishi katika maeneo ya mabonde kuhama maeneo hayo hasa wakati huu ambapo nchi inashuhudia mvua kali ili kuepuka maafa zaidi.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.